[Latest Updates]: Wadau wa Madini Shinyanga wanufaika na uwepo wa Soko la Madini

Tarehe : March 12, 2025, 1:27 a.m.
left

Wadau wapongeza uwepo wa ubao wa kidigitali wa kuonesha bei elekezi za madini


Wadau wa madini  wakiwemo wachimbaji, wachenjuaji na wafanyabiashara wa madini katika mkoa wa Shinyanga wamepongeza uwepo wa Soko la Madini-Shinyanga, ambalo tangu kuanzishwa kwake limekuwa msaada mkubwa ambapo madini yanauzwa kulingana na bei elekezi inayoendana na soko la dunia ambayo huoneshwa kwenye ubao maalum wa kidigitali.

Akizungumza leo Machi 12, 2025 katika soko hilo, Afisa kutoka Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Shinyanga,  Shikimayi Muyinza amesema, soko hilo limekuwa na tija kubwa kwa wachimbaji na wafanyabiashara   wa madini mkoani humo ambapo Serikali imeweka utaratibu mzuri wa kutoa bei elekezi na kuepusha changamoto za wachimbaji kupunjwa kwa kupewa bei ndogo na baadhi ya  wafanyabiashara wasio waaminifu.

 “Ikiwa ni sehemu ya kuboresha huduma, Soko hili linatumia ubao unaotumia teknolojia ya kidigitali ambao unaonyesha bei elekezi za madini ya dhahabu sambamba na madini mengine  kama vile shaba na fedha ili kuongeza uwazi  kwenye shughuli za biashara hapa sokoni tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo bei elekezi iliyokuwa inatolewa ni ile ya madini ghafi ya dhahabu tu ”amesema Muyinza.

Aidha, baadhi ya wadau wa madini mkoani Shinyanga wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Wizara ya Madini pamoja na Tume ya Madini kwa hatua ya uanzishwaji na usimamizi wa masoko ya madini na vituo vya ununuzi wa madini kwani yameleta mabadiliko ya kiuchumi katika Mkoa wa Shinyanga ikiwa ni pamoja na ajira, mapato kwa Serikali na kuongeza kasi ya ukuaji wa shughuli za uchimbaji wa madini katika mkoa huo.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals