[Latest Updates]: TARURA Geita Yahudumia KM 564 Maeneo ya Madini

Tarehe : Sept. 25, 2025, 11:21 a.m.
left

TANESCO, RUWASA na NIRC yanufaika na Maabara ya Kisasa ya TARURA-Geita

Elimu ya Fidia yatolewa kwa wananchi

Geita

Wakala ya Barabara za Vijijini ma Mijini (TARURA) Mkoa wa Geita inahudumia  mtandao wa barabara upatao Km. 7274  na kati ya hizo Km. 564 ya barabara zinazohudumia maeneo ya madini.

Hayo yamebainishwa na Meneja wa TARURA Mkoa wa Geita Mhandisi David Msechu wakati akiongea na waandishi wa habari katika Maonesho ya Nane ya Madini yanayoendelea Mkoani hapa.

Amesema katika mtandao huo asilimia 60 ya barabara zinapitika  hivyo maonesho hayo licha ya kutoa elimu kwa umma,wanashiriki kikamilifu kuhakikisha wanaendeleza ukuaji wa uchumi pamoja na kuendeleza huduma za jamii kwa kuhudumia barabara zinazoelekea maeneo ya migodini.

Aidha, Mhandisi Msechu amesema kwa mwaka wa fedha 2024/2025 na 2025/2026 wametenga kiasi cha shilingi milioni 580 kwa ajili ya kukamilisha Km. 210  zikiwemo barabara zinazoelekea migodini.

Kwa upande mwingine Mhandisi Msechu amesema TARURA Geita wana Maabara ya kisasa ambayo inapima ubora wa vifaa vya ujenzi wa miundombinu ya barabara pamoja na miundombinu mingine inayotekelezwa na  Taasisi nyingine zikiwemo TANESCO, Tume ya Umwagiliaji pamoja RUWASA  ambayo inatumia maabara hiyo kutekeleza miradi yao kwa ubora unaohitajika.

Naye, Mhandisi wa Miradi kutoka TARURA Makao Makuu Faizer Mbange amesema wanatumia maonesho hayo kutoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi sahihi ya barabara ikiwemo kutokupitisha wanyama kwenye barabara, kulinda na kutunza barabara, kuepuka kulima kandokando ya barabara pamoja na kutopitisha mizigo mizito kwenye barabara.

Amesema wananchi wengi waliotembelea banda la TARURA baadhi yao walikuwa na changamoto ya kutoelewa masuala ya fidia hivyo wameweza kutoa elimu hiyo pia.

“TARURA inatekeleza miradi kwa fedha za ndani pamoja na ile ya fedha za ufadhili hivyo ipo baadhi ya miradi ambayo ina fidia”.

Ameongeza kusema kwamba TARURA pia imeweza kutoa elimu ya uanzishaji wa vikundi kazi kwa ajili ya matengenezo madogo madogo ya barabara  ambapo vikundi hivyo huhusika pia katika ulinzi wa barabara hizo.
-Mwisho-

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals