[Latest Updates]: Kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma

Tarehe : June 23, 2023, 10:26 a.m.
left

Katika kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo hufanyika Barani Afrika tarehe 16 hadi 23 Juni ya kila mwaka, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo amewatembelea na kuzungumza na Watumishi wa Wizara ya Madini Makao Makuu katika maeneo yao ya kazi, jijini Dodoma.

Ziara hiyo fupi iliyofanyika leo Juni 22, 2023, imelenga kusikiliza changamoto, kero, kupata maoni, ushauri na mapendekezo   kutoka kwa mtumishi mmoja mmoja  wa Idara na Vitengo wizarani  ili kuboresha mazingira ya kazi, maslahi ya watumishi kwa maendeleo ya Sekta ya Madini.

Akizungumza katika ziara hiyo, ambayo ameitaja kama Wiki ya kufungua milango, Naibu Katibu Mkuu Mbibo amewataka watumishi kufahamu  matarajio makubwa waliyonayo wananchi kuhusu Sekta ya Madini na hivyo kuwasisitiza kufanya kazi kwa bidii, weledi na tija na  ili kuiwezesha Sekta ya Madini kubadilisha uchumi wa taifa.

‘’ Jamii ya watanzania inaona kabisa rasilimali madini zinaweza kubadili uchumi wa Tanzania na wanayo matarajo makubwa na Sekta hii. Ni vema tukakidhi malengo hayo kwa asilimia inayotekelezeka,’’ amesisitiza Mbibo.

Aidha, amewaeleza watumishi hao  kuwa  ziara yake imelenga  kusikiliza ili hatimaye kuimarisha mazingira ya  kazi na kuondoa changamoto  ambazo zinahitaji  utatuzi wa haraka  kwa lengo la kuongeza motisha na tija  ya kazi kwa maendeleo ya Sekta ya Madini, na kuongeza kwamba, changamoto zinazohitaji taratibu zaidi  za  Kiserikali zitafanyiwa kazi.

Vilevile, mbali ya kuwatembelea watumishi,  Mbibo ametoa nafasi kwao  kuwasilisha kero, changamoto, maoni na ushauri katika ofisi yake na kueleza kuwa, mlango wake uko wazi kuwapokea watumishi ili kuwasilikiza.

Pia, amezungumzia umuhimu wa watumishi kushiriki katika mazoezi na michezo mbalimbali inayoandaliwa na wizara ili kuimarisha afya zao na kutumia fursa hiyo kumpongeza Mtumishi wa wizara ya Madini mwanamichezo mahiri Hilda Masanche  ambaye ameteuliwa katika Kamati ya Ufundi ya CECAFA katika mashindano  ya CECAFA ya wasichana chini ya miaka 18. Mbali ya kuwa kwenye kamati hiyo Hilda ni Kocha Msaidizi katika  timu za taifa Twiga Stars  kwa wachezaji wa chini ya miaka 17 na miaka 20

Pongezi hizo zimetolewa  na Mbibo kufuatia mtumishi huyo kuishukuru wizara kwa kumpa fursa na nafasi ya kushiriki katika shughuli za michezo mbalimbali ambapo amekuwa akiliwakilisha taifa.

Wakizungumza wakati wa  ziara hiyo wafanyakazi kutoka kada mbalimbali wizarani, wameupongeza uongozi wa wizara kwa kutenga muda wao kuwatembelea katika maeneo yao  ikiwemo kuwapatia wasaa wa kusikiliza changamoto, kero na kupokea ushauri na maoni yao.

Mbali ya kuwatembelea watumishi katika maeneo yao ya kazi ili kuwasikiliza, Wizara ya Madini imeweka dawati maalum ili kutoa fursa kwa wageni na watumishi kujifunza kuhusu majukumu mbalimbali yanayotekelezwa na wizara ikiwemo kupatiwa nafasi ya kutoa maoni na mapendekezo yote yakilenga kuimarisha na kuboresha mazingira ya kazi, hali za watumishi na maendeleo ya sekta ya Madini kwa Ujumla.

Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma huenda Sambamba na Kaulimbiu ambapo mwaka 2023 Kaulimbiu inasema ‘’ Kufanikiwa  kwa eneo huru la Biashara Barani Afrika (Acfta) kunahitaji Usimamizi wa Utumishi wa Umma wenye Mtazamo wa Kikanda.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals