[Latest Updates]: Mabadiliko ya Sheria ya Mwaka 2017 Yaipaisha Sekta ya Madini

Tarehe : Sept. 22, 2020, 11:04 a.m.
left

Tito Mselem na Steven Nyamiti, Geita

Imeelezwa kuwa, Sekta ya Madini, imefanikiwa katika usimamizi wake kufuatia mabadiliko ya Sheria yaliyofanywa mwaka 2017 chini ya uongozi wa Rais, John Pombe Magufuli na kuifanya Sekta hiyo kuongoza katika ukuaji kwa asilimia 17.7.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Madini Doto Biteko wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Geita ambapo alisema Sekta ya Madini imeongoza kwa ukuaji kwa asilimia 17.7 na ndiyo Sekta inayoongoza kwa kuiletea Serikali fedha za kigeni.

Waziri Biteko amesema kuwa, Sekta ya Madini inaongoza kwa kusafirisha bidhaa kwenda nje ya nchi ambapo asilimia 51.9 ya bidhaa zote zinazo safirishwa nje ya nchi zinatokana na Sekta ya Madini.

Vilevile, Waziri Biteko amesema kuwa, mapato yatokanayo na Sekta ya Madini yamepanda kutoka bilioni 168 kwa mwaka mpaka kufikia bilioni 528.

Imeelezwa kuwa ndani ya mabadiliko ya Sheria ya Madini ya mwaka 2017 kuna kipengele kinachoeleza kuwa kampuni zote zinazo chimba madini nchini Tanzania lazima zifungue akaunti zake ndani ya nchi.

Kampuni ya Barrick iliyoingia ubia na Serikali na kutengeneza kampuni ya pamoja inayoitwa Twiga imefungua akaunti zake zote hapa nchini ambapo mkataba huo ulisainiwa tarehe 24 januari, 2020.

Pia, Waziri Biteko amesema kuwa, Makinikia yanayo safirishwa nje ya nchi yanakuwa yamesha nunuliwa hapa nchini na kuyapima kwenye maabara tatu tofauti ili kujiridhisha kiwango na aina za madini yaliopo kwenye makinikia hayo na fedha zote zinawekwa kwenye banki za hapa nchini tofauti na ilivyokuwa awali

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals