[Latest Updates]: STAMICO Yapeleka Tabasamu Kwa Watu Wenye Mahitaji Maalum Hombolo

Tarehe : Dec. 25, 2025, 11:52 a.m.
left

MD STAMICO  awazindulia mradi mkubwa wa Kuku wa Mayai
Changamoto za kupata matibabu kwa wahitaji na wazee  hawa  zapatiwa suluhisho kwa kupewa kadi za Bima ya Afya.
Wafurahia kupata chakula pamoja na walezi wao wa STAMICO.

Hombolo, Dodoma 

 Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) katika utaratibu wake wa kawaida wa kusaidia makundi  yenye uhitaji  kwenye  jamii, jana tarehe 24 Disemba 2025 walishiriki katika chakula cha pamoja na wahitaji wa Kikundi cha Hombolo.

Akizungumza kabla ya kushirki katika chakula hicho, Dkt Venance Mwasse, Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO  aliwazindulia Mradi mkubwa wa Ufugaji wa Kuku wa Mayai  kuwasaidia kupata kipato cha kuweza kujikimu kwenye mahitaji yao ya kila siku.
Katika hotuba yake, Dkt Mwasse  alielezea dhamira yake ya  kuona Wazee  na Wahitaji  wa kijiji cha Samaria, wanaishi na uso wa furaha, tabasamu, na Kicheko na ameahidi kuwa Samaria itakuwa "American Garden" kwa Mapumziko. Hii ndo sababu ya kuzindua mradi wa Ufugaji wa kuku ili kuweza kuondoa janga la Umasikini kwa Wanasamaria.  Aliongeza kupitia STAMICO, wazee wa Samaria, familia zao na wenye ulemavu  katika kikundi cha Hombolo sasa  watapata matibabu bure kupitia mpango ambao unaratibiwa  na  NSSF. STAMICO  imeshawalipia ada ya miezi 3  ambayo ndio inatakiwa ili waweze kuingia  katika mpango huo unaowawezesha kutibiwa katika hospitali ndogo na kubwa kama Hospitali ya Benjamini Mkapa.

 Akiongea katika hafla hii, mwakislishi wa Mkurugenzi wa NSSF ndugu John alimpongeza sana MD wa STAMICO kwa kazi nzuri na utayari wa kuwasaidia wahitaji hawa. Alisema  MD anafanya kazi nzuri  na anamwakilisha ipasavyo Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na utendaji kazi wake ambao hauwaachi nyuma makundi ya watu wenye mahitaji maalumu.

 Upatikanaji wa bima hii, utasaidia kuboresha afya za wazee wa Samaria na Wanasamaria. Mwakilishi wa Mkurugenzi wa NSSF ameahidi mbele ya MD wa STAMICO kuendelea kushirikiana ili kuhakikisha Wanasamaria wanaishi maisha mazuri zaidi.

 Dkt Mwasse amewahakikishia Wanasamaria kuwa Mapema mwezi wa Kwanza 2026, Umeme utakuwa umewaka eneo la Samaria. Hii yote ni katika kuhakikisha kuwa Samaria inakuwa mahala pa Bustani ya Raha na Faraja (American garden)

Baada ya  hotuba  ya MD na kuzinduliwa kwa  mradi wa Kuku wa Mayai, MD  wa STAMICO  aliungana na Wafanyakazi wa STAMICO pamoja na Kikundi cha Wanawake na Samia wa  Mkoa wa Dodoma kushiriki katika chakula cha Pamoja na Wanasamaria ikiwa ni siku moja kabla ya Sikukuu ya Krismasi. Lengo  kuu ilikuwa  kuhakikisha Wahitaji wa Samaria wanajiona kuwa na wao wanasherekea sikukuu hii kwa kula na kunya pamoja na jamii zingine. 

Wazee wa Samaria wakiwa na nyuso za furaha walimshukuru MD wa STAMICO na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa NSSF kwa kuwa sehemu ya faraja na Furaha kwa wazee wa Samaria. Charles Chiboko, alimshuruku Dkt  Mwasse kwa kuwajali wazee mara kwa mara na wataendelea kumuombea zaidi kwa Mungu ampe uhai, uzima na nguvu. Naye Bibi Roza Ufinyu alimpongeza na Kumshukuru Dkt Mwasse kwa kuendelea  kuwakumbuka kila inapofika kipindi hiki cha  Krismasi  na  pia  kuwaletea mardi wa kufuga Kuku wa Mayai Samaria..

STAMICO  inaendelea na utaratibu  wa  kuhakikisha pamoja na majukumu yake inatenga muda na rasilimali za kuwasaidia wahitaji kwenye Jamii

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals