Tarehe : June 28, 2025, 2:37 p.m.
Asisitiza umoja na mshikamano
Eng.Samamba asema Bonanza limelenga kumarisha afya, kujenga mshikamano
Dodoma
Waziri wa Madini Mhe.Anthony Mavunde amewataka Watumishi wa Wizara na taasisi zake kuendeleza utamaduni wa kufanya michezo ya pamoja na kueleza kuwa inasaidia kuimarisha afya na utendaji kazi za Wizara.
Ameyasema hayo leo Juni 28, 2025 wakati akifungua Bonanza la Wizara ya Madini na Taasisi zake lililofanyika katika Viwanja vya Shule Sekondari John Merlin, jijini Dodoma.
Ameongeza kuwa, Sekta ya Madini imeendelea kufanya vizuri katika maeneo mbalimbali ikiwemo mchango wake kwenye Pato la Taifa na kutumia nafasi hiyo kumshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na maelekezo na miongozo yake ambayo inaifanya Sekta kuendelea kupiga hatua.
Pia, amemshukuru Katibu Mkuu Wizara ya Madini Eng.Yahya Samamba
kwa ushirikiano wake na kuendeleza michezo ya pamoja suala ambalo linachochea umoja miongoni mwa watumishi na kuongeza tija kwenye kazi.
"Nawashukuru sana watumishi wa Wizara na taasisi zake katika kipindi changu cha miaka miwili kasoro ndani ya Wizara sote tumefanya vizuri. Hata jana Mhe. Rais alipofunga Bunge alizungumzia kuhusu Sekta ya Madini kuendelea kufanya vizuri.Sifa huwa zinarudi kwetu lakini ninyi ndiyo wafanyakazi," amesema Mavunde.
Amesisitiza kuhusu watumishi kuendelea kufanya kazi kwa bidii ikizingatiwa kwamba Mwaka wa Fedha 2025/26 Wizara imewekwa malengo makubwa ambayo yanapaswa kutekelezwa kwa manufaa ya taifa kiuchumi.
"Tuendelee tuliposhia ili Sekta itoe mchango zaidi na siku moja iwe Sekta kinara kiuchumi nchini," amesema Waziri Mavunde.
Akizungumza katika bonanza hilo, Katibu Mkuu Wizara ya Madini Eng. Yahya Samamba amesema kwamba kufanyika kwa bonanza hilo ni utekelezaji wa maelekezo ya Waziri Mavunde ambaye kipindi ameteuliwa kuingoza Wizara aliomba Wizara watumishi wa Wizara na taasisi kukutana pamoja kupitia michezo ili kujenga umoja na ushirikiano miongoni mwa watumishi.
Naye, Kamishna wa Madini Dkt. Abdul Rahman Mwanga amempongeza Waziri Mavunde kwa kuisimamia Sekta vizuri na kusema, "ni matamanio yangu upite na urudi tena kuendeleza tulipoishia,".
Bonanza hilo limeaongozwa na kaulimbiu isemayo
Michezo ni furaha: Shiriki Uchanguzi 2025
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.