[Latest Updates]: Waziri Mavunde Azindua Mradi wa Kihistoria wa Vijana Nyamongo - Tarime

Tarehe : May 3, 2025, 10:02 p.m.
left

Agawa Leseni za madini awamu ya kwanza kwa Vijana 2000

Ni utekelezaji wa Maagizo ya Mh. Rais Dkt. Samia

Aupongeza mgodi wa Barrick North Mara kwa kutoa Leseni kwa Vijana wa Vijiji 13 

Benki ya Dunia (WB) na Baraza la Dhahabu Duniani (WGC) waonesha dhamira kusaidia mradi

Tarime,Mara

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde  amezindua mradi wa uchimbaji Madini ya dhahabu kwa vijana, wanawake na wenye ulemavu kwa kutoa leseni za uchimbaji mdogo wa madini ikiwa ni utekelezaji wa Programu ya Mining For a Brighter Tomorrow (MBT).

Amezindua mradi huo leo Mei 03, 2025 katika viwanja vya shule ya sekondari Ingwe vilivyopo katika eneo la Nyamongo wilayani Tarime  Mkoa wa Mara ambapo ametoa leseni 48 za uchimbaji mdogo wa madini kwa wanufaika zaidi ya 2000 vijana, wanawake na wenye nahitaji maalumu.

Akizungumza katika hafla hiyo amesema, Wizara ya Madini imekamilisha maandalizi ya Programu ya MBT ambayo itatekelezwa katika kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2025 hadi 2030 ambapo Programu hiyo ni ya kimageuzi katika Sekta ya Madini ambayo imeanzishwa kwa ajili ya kushughulikia changamoto na kuboresha fursa kwa wanawake, vijana na watu wenye mahitaji maalum ili kuongeza ushiriki wa makundi hayo katika mnyororo wa thamani wa madini.

"Naomba nichukue fursa hii kumpongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye yeye alitupa maelekezo kuhakikisha vijana, wanawake na wenye mahitaji maalumu wanashiriki kikamilifu katika shughuli za madini.

Naupongeza Mgodi wa Barrick North Mara kwa kutoa Leseni kwa Vijiji 13 ambazo zitaendana na msaada wa kiufundi kwa Vijana zaidi ya 2000 watakanaonufaika na mradi huu.

 Tukio hili litasaidia kuondoa mahusiano hasi kati ya mgodi wa North Mara na wananchi wanaozunguka mgodi huo ambao walionekana mara kadhaa kuvamia mgodi huo.

Mradi huu wa kihistoria na wa kwanza kufanyika nchini baina ya serikali,Mgodi na wananchi wanaozunguka mgodi,umevutia ushiriki mkubwa wa wadau kama Benki ya Dunia(WB) na Baraza la Dhahabu Duniani(WGC) ambao wameonesha dhamira ya kusaidia utekelezaji wake.”Alisema Mavunde

Meneja Mkuu wa Mgodi wa North Mara Mhandisi Apolinary Lyambiko amesema utoaji wa Leseni hizo una lengo la kuimarisha uhusiano mwema na jamii inayozunguka  mgodi.

Akitoa salamu zake,Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini Mh. Mwita Waitara ameipongeza serikali pamoja mgodi kwa mradi huu ambao utatoa ajira nyingi kwa vijana wa Tarime na kuiomba serikali isaidie upatikanaji wa mitaji wa kuendesha shughuli za madini.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evance Mtambi amempongeza Waziri Mavunde kwa namna anavyo  wasaidia wananchi wa Mara hususan katika eneo la Sekta ya Madini ambapo amesema juhudi za Waziri huyo zinaonekana kwa vitendo na kuomba vijana hao wajengewe uwezo ili waweze kuchimba kwa tija.

Sambamba na hayo, Kanali Mtambi amemuomba Waziri Mavunde kutoishia kwenye utoaji wa leseni pekee bali pia kuliangalia suala la msaada wa kiufundi pamoja na mitaji ili kuwawezesha wachimbaji hao kufanya kazi kwa tija.

Naye, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo Tanzania (FEMATA), John Bina amempongeza Waziri Mavunde kwa kuzindua mradi huo na kuwataka vijana, wanawake na wenye mahitaji maalumu kufanya kazi kwa kushirikiana na kuepuka migogoro isiyo ya lazima.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals