[Latest Updates]: Marufuku Biashara ya Madini Kufanyika Hotelini – Dkt. Kiruswa.

Tarehe : Dec. 17, 2023, 6:15 p.m.
left

Naibu Waziri wa Madini, Dkt Steven Kiruswa amepiga marufuku wageni kutoka nje ya nchi kununuwa madini wakiwa hotelini kwani kwa kufanya hivyo ni kuvunja sheria hivyo wanapaswa kuchukuliwa hatua ikiwa nia pamoja na kukamatwa na kushtakiwa.

Dkt. Kiruswa alisema hayo katika Kijiji cha Mundarara chenye sifa ya uchimbaji madini ya Ruby kilichopo katika wilaya ya Longido mkoani Arusha wakati akiongea na wawekezaji wa madini hayo, viongozi wa vijiji vyote vya kata ya Mundarara na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Longido.

 

Alisema ni kosa kisheria mgeni kufanya biashara akiwa hotelini kwani serikali lazima itakuwa inakosa mapato kwani hakuna uhakika rasmi wa biashara hiyo  inayofanyika huko kwa kificho na kanuni na sheria za madini haziruhusu mgeni kufanya biashara ya madini bila ya kuwa na mbia mzawa.

Dkt. Kiruswa aliwataka wafanyabiashara wa madini ya Ruby na madini mengine nchini kuacha mara moja tabia hiyo ya kuhifadhi wageni hotelini na kufanya biashara haramu ya kununua madini kwa kijicho kwani dola haitawacha salama.

Alisema kuwa Serikali imejenga mazingira mazuri ya kufanya biashara ya madini kwa wawekezaji, wachimbaji wakubwa na kati na wachimbaji wadogo lakini inasikitisha kuona bado watu hawaridhiki na mazingira hayo sasa serikali haitakuwa na huruma kwa wale wenye nia ovu yenye lengo la kujitajirisha na kuvunja sheria.

Dkt. Kiruswa alisema Serikali iko macho na inajua kila kitu na wakati ukifika wale wote wenye kufanya biashara haramu ya madini dola itawakamata kwani hawana nia njema na Serikali.

‘’Ukikutwa umemhifadhi mgeni hotelini na unashirikiana naye kufanya biashara ya kununuwa madini na kwenda kuuza nje bila kufuata sheria serikali haitakuacha salama lazima ushughulikiwe kisheria kwani wewe ni muhujumu uchumi’’ alisema Kiruswa

Akizungumzia utoroshaji wa madini nje ya nchi kwa njia ya panya,Waziri Kiruswa aliwataka wawekezaji wa madini ya Ruby  na madini mengine kuacha mara moja kwani kufanya hivyo ni kukiuka taratibu na watashikwa kwani dola iko kila mahali na inafuatilia nyendo zote kwa ukaribu.

Dkt Kiruswa alisema serikali inajitahidi kila kukicha kujenga mazingira mazuri ya wachimbaji madini na wafanyabiashara wa sekta hiyo lakini kuna baadhi yao hawana nia njema kazi kupanga mikakati haramu ya kufanya biashara haramu ikiwa ni pamoja na kutorosha madini bila kufuata taratibu.

Alisema kwa sasa hilo halitavumiliwa na kuwatahadharisha wafanyabiashara wa madini kote nchini kuacha mara moja tabia ya kutorosha madini nje kunainyima serikali kuongeza mapato katika sekta hiyo.

Aidha, Dkt. Kiruswa aliwashukuru viongozi wa bodi ya Mgodi wa Ruby Unaomilikiwa na Kijiji cha Mundarara kwa kumaliza mgogoro na Mwekezaji Mzawa Rahimu Mollel maarufu kwa jina la Pendeza kwa kukaa pamoja na kuondoa tofauti zilizokuwa zikijitokeza na kwa kufanya hivyo kunaweza kuleta maendeleo katika Kijiji hicho kwa maslahi ya wanachini wote.

Sambamba na hilo, Dkt. Kiruswa alimtaka Afisa madini Mkoa wa Arusha {RMO} kushughulikia changamoto za wachimbaji madini ya Ruby kwa wakati ili kujenga imani kwa wachimbaji na serikali yao kuliko kukaa muda mrefu bila kutatua changamoto zinazowakabili kwani kunaweza kuleta sitafamu ambayo haina msingi.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals