[Latest Updates]: Biteko atatua mgogoro wa leseni uliodumu kwa miaka 10

Tarehe : April 28, 2018, 11:52 a.m.
left

Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko ametatua mgogoro wa Leseni ya Madini uliodumu kwa takribani miaka kumi kwa kuamuru kupitia haraka eneo la leseni ya uchimbaji wa Madini kwa Wachimbaji wadogo wa Chama cha Ushirika cha Kasi Mpya Gold Mine.

Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko akikagua maeneo ya uchimbaji baada ya mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Mwazimba, Kata ya Chela, Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga.[/caption]

Biteko alitoa agizo hilo wakati akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini waliohudhuria kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Mwazimba, Kata ya Chela, tarehe 3 Februari, 2018.

Naibu Waziri Biteko alifanya ziara hiyo kufuatia malalamiko ya wachimbaji wadogo yaliyowasilishwa Wizara ya Madini mjini Dodoma tarehe 26 Januari, 2018, na Mbunge wa Jimbo la Msalala Ezekiel Maige.

Alisema kuwa, wananchi walifunga safari mpaka Ofisi za Madini kwa ajili ya kupata uhalali wa kupimiwa eneo lao kwa kutumia GPS lakini Kaimu Afisa Madini Mkazi Wilaya ya Kahama akawabadilishia Nukta (Coordinator) ambazo baadaye zilionekana kuwa za eneo jingine ambalo ni mbuga isiyokuwa na madini huku eneo hilo likihamishiwa kwa mtu mwingine.

Kutokana na hilo, Biteko alimuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini kumchukulia hatua za haraka za kinidhamu aliyekuwa Kaimu Afisa Madini Mkazi Wilaya ya Kahama aliyehusika na upotoshaji wa leseni na kuzua mgogoro wa usumbufu usiokuwa na sababu dhidi ya wananchi na Serikali.

Alisema kuwa, hakuna sababu ya Wizara ya Madini kukumbatia mgogoro huo wa leseni uliodumu kwa miaka kumi kwa sababu ya eneo ambalo lilipotoshwa na baadhi ya watendaji wa Wizara ya madini kwa kuwa jukumu la Serikali ni kuwatumikia wananchi ikiwemo utatuzi wa migogoro mbalimbali zinazowakabili katika jamii.

Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko akikagua maeneo ya wachimbaji wadogo wa Chama Cha Ushirika cha Kasi Mpya Gold Mine katika Kijiji cha Mwazimba, Kata ya Chela, Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga.[/caption]

Pia, Biteko aliwataka wachimbaji wadogo kuwa waaminifu na kufichua baadhi ya wachimbaji wanaoficha madini kwa lengo la kuyatorosha bila kulipa kodi.

Aidha, aliongeza kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli haitawafumbia macho wamiliki wa leseni ambao leseni zao zimedumu kwa muda mrefu bila kuzifanyia kazi kwa kuwa hazizalishi ajira yoyote wala kulipa kodi na kuongeza kuwa, Serikali imekusudia kuzifuta na kuwapa watu wengine ambao watazifanyia kazi.

Alitoa mfano kuwa, katika eneo la Kahama kuna leseni 249 lakini zinazofanyiwa kazi ni 18 tu huku wenye leseni zisizofanya kazi wakisubiri wachimbaji wadogo waanze kuchimba madini na baadaye kuwaondoa kwa kisingizio cha umiliki wa leseni wakati zikiwa zimedumu kwa muda mrefu bila kuendelezwa.

Aidha, alisema kuwa tayari Serikalia imetenga maeneo makubwa manne (4) kwa ajili ya wachimbaji wadogo ikiwemo eneo la Nyang'wale lenye hekari 996, eneo la Nyangarata lenye hekari 1074, Eneo la Buzwagi kilometa za mraba 53.4 na eneo la Kinamyuba kilomita za mraba 33.3.

Aliongeza kuwa, jukumu la Serikali ni kutatua kero za wananchi na si kuwaongezea kero, hivyo, watendaji wote wa Serikali wanapaswa kutimiza ndoto ya Rais Magufuli ya kuwatumikia wananchi.

Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko, akikagua maeneo ya wachimbaji wadogo wa Chama cha Ushirika cha Kasi Mpya Gold Mine katika Kijiji cha Mwazimba, Kata ya Chela, Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga.[/caption]

Sambamba na hayo, Naibu Waziri Doto Biteko aliwataka wananchi kuendelea na uchimbaji wakati taratibu zikifuatwa ili kukamilisha mgogoro huo huku akiwahakikishia kutoondolewa tena na endapo watahitaji maeneo mengine yaliyotengwa kwa ajili ya wachimbaji wadogo wanapaswa kufuata taratibu za kisheria zilizoainishwa.

Awali, Mbunge wa Msalala Ezekiel Maige alimweleza Naibu Waziri kuwa wananchi wake wameonewa kwa muda mrefu ikiwemo yeye kufutailia mgogoro huo bila mafanikio.

“Ni kwasababu ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Magufuli kuwa kimbilio la wanyonge, mheshimiwa Naibu Waziri nilikua nimekata tama,” alisema Maige.

Na Mathias Canal, Shinyanga

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals