[Latest Updates]: Tumelenga Kuifanya Tanzania Kitovu cha Madini Afrika - Kheri Mahimbali

Tarehe : Feb. 6, 2024, 7:58 a.m.

 

Zambia Yafurahishwa na Utaratibu wa  Wizara Kukutana na Wawekezaji Kila Robo Mwaka

Capetown

Katibu Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali amesema Tanzania imelenga kuwa Kitovu cha Madini Barani Afrika sababu ambayo imepelekea Serikali kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji katika Sekta ya Madini.

Ameongeza kwamba, Wizara imeweka utaratibu wa kukutana na kampuni  kubwa na za kati zilizowekeza katika miradi ya madini nchini kila robo ya mwaka ili kujadili na kutatua kero ambazo zinaweza kusababisha ucheleweshaji wa masuala yanayohusu uwekezaji na  kuongeza kuwa, tayari wizara imekwishateua maafisa maalum ambao ni mabalozi wa kila mradi hiyo.

Mahimbali ameyasema hayo Februari 6, 2024 wakati akichangia katika mdahalo maalum uliolenga kujadili ufunguaji wa fursa za uwekezaji katika Sekta ya Madini na namna ya kukabiliana na changamoto zinazopelekea kukwamisha uendelezaji wa miradi mikubwa ya madini katika nchi za Afrika, kwenye mkutano wa  Uwekezaji wa Mining Indaba unaoendelea nchini Afrika Kusini.

Akizungumza katika mdahalo huo, mmoja wa wachangiajia katika mdahalo huo kutoka Ofisi ya Rais ya Serikali ya  Jamhuri ya Zambia Jito Kayumba, ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuanzisha utaratibu wa kukutana na wawekezaji na kuongeza kuwa,  Tanzania imekuwa mfano kwa nchi hiyo kujifunza masuala mbalimbali  yanayohusu usimamizi wa sekta ya madini na kuziasa nchi nyingine kujifunza pale wanapoona kuna jambo la kipekee kutoka sehemu nchi nyingine.

Kwa nyakati tofauti viongozi wakuu wa wizara,  wamekutana na kampuni mbalimbali zilizowekeza nchini pamoja na kampuni kadhaa zinazoshiriki katika mkutano huo ambazo zinakutana na Wizara ili kuendelea kupata taarifa za kina zinazohusu uwekezaji katika Sekta ya Madini nchini.

 Kampuni ambazo leo zimekutana na viongozi wa Wizara ni pamoja na MANTRA Tanzania, Tesla, AngloGold Ashanti, BHP na Life Zone Metals, Taasisi ya Jiolojia ya Uingereza  na kampuni ya JOGMEC ya Botswana.

 Aidha, vikao hivyo vimetanguliwa na kikao kilichohusisha Chemba ya Migodi Tanzania, kampuni zilizowekeza nchini pamoja na kampuni zilizovutiwa na taarifa za uwekezaji za Tanzania.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals