Tarehe : July 7, 2025, 12:40 p.m.
Dar aEs Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse amesema ushiriki wa pamoja wa Wizara taasisi zake pamoja na wadau wa Sekta ya Madini katika banda la shirika hilo umeongeza tija kwa kuwa umewarahishia wageni kupata taarifa zote kwenye mnyororo wa shughuli za madini.
Amebainisha hayo leo Julai 7, 2025 baada ya kutembelea banda hilo ambapo
ameonesha kufurahishwa na idadi kubwa ya wageni wanaotembelea banda huku wakionesha kufurahia huduma na elimu wanazozipata.
"Ni jambo la kufurahisha kuona banda limetembelewa na wageni wengi ambao wanapata taarifa kutoka kwa wataalam na watoa huduma mbalimbali," amesema Dkt. Mwasse
Kufuatia hali hiyo, ametoa wito kwa wananchi kufika ndani ya banda hilo kutokana na uwepo wa taarifa za kutosha ikiwemo fursa zilizopo katika Sekta ya madini.
Aidha, ameweza kukutana na
wataalam mbalimbali wanaoshiriki maonesho hayo kupitia banda hilo.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.