[Latest Updates]: Waziri Mavunde Akutana na Uongozi wa Mamba Minerals Corporation na Kampuni ya Peak Resources Ngualla

Tarehe : April 18, 2024, 3:14 p.m.
left

Dodoma

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amekutana na  Mtendaji Mkuu wa Kampuni  ya Peak Resources Ngualla Company ya nchini Australia ( PRNG) Bw. Bardin Davis,  yenye umiliki wa hisa asilimia 84% kwenye mradi wa Uchimbaji Madini  Mkakati ya Rare Earth Elements.

Katika kikao hicho kilichofanyika  Aprili 18, 2024 jijini Dodoma,  Bw. Bardin ameambatana  na Afisa Mkuu   wa masuala ya Fedha ya kampuni hiyo  Bw. Phil Rundell,  pamoja na Mkurugenzi wa Mamba Minerals Corporation  Limited ( MML)   yenye ubia na Serikali, Bw. Ismail Diwani.

Katika kikao hicho, Mtendaji Mkuu wa PRNG Bw. Bardin  amemweleza Waziri Mavunde kuhusu maendeleo ya mradi huo na kueleza kuwa  hivi sasa upo katika hatua ya kufanya tathmini ya fidia ya wananchi wanazunguka mgodi ikiwemo uendelezaji wa utafiti wa madini ya mkakati aina ya niobium, fluorspar na phosphate. 

Aidha, Bardin ametumia kikao hicho  kuishukuru Wizara kupitia Tume ya Madini kwa  kuridhia kuongeza ukubwa wa leseni ya kampuni hiyo.

Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Mavunde ameusistiza uongozi wa kampuni  hiyo  kufuata masharti ya leseni  waliyopewa ikiwa ni pamoja na kuzingatia matakwa ya Sheria ya Madini na kusisitiza kuhusu umuhimu wa madini hayo  kusafishwa hapa hapa  nchini.

Madini ya rare earth elements  yanayotumika kutengeza sumaku kwenye mota za magari ya umeme , betri za magari ya mseto na umeme;na  vitu vingine  mbalimbali vya umeme. 

Kampuni ya Mamba Minerals  inayomiliki leseni kubwa ya uchimbaji  yenye jina la Rare Earth Elements ilitolewa tarehe 25 Aprili, 2023.

Mradi wa uchimbaji madini hayo upo kijiji cha Ngualla, Mkoani Songwe.

Katika mradi huo, Serikali ya Tanzania ina miliki  asilimia 16 za hisa zisizohamishika.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals