[Latest Updates]: Mbibo Afurahishwa na Ubunifu wa Makusanyo, Njombe

Tarehe : March 16, 2022, 1:09 p.m.
left

Imeelezwa kuwa,  makusanyo yameongezeka kufikia asilimia 93 katika kipindi cha miezi 9 katika ofisi ya madini Njombe.

Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Msafiri Mbibo wakati akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Madini  Mkoa wa Njombe.

"Nimefurahishwa na jinsi Ofisi ya Madini inavyoratibu shughuli zake na hasa ubunifu sahihi unaofanywa wa njia za kuongeza makusanyo," amesema.

Aidha, amesisitiza  watumishi kuendeleza juhudi katika ukusanyaji wa mapato ili wavuke lengo baada ya kufunga mwaka wa fedha 2021/2022.

Akizungumzia ushirikiano, Mbibo amewaeleza kuwa, Wizara ya Madini itaendelea kushughulikia changamoto za watumishi zilizowasilishwa kwake ili kuongeza ufanisi wa kazi katika ofisi hiyo. Kwa upande mwingine, amewataka  wafanye kazi kwa bidii ili Sekta ya Madini iongeze tija kwa Taifa. 

Naye Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Njombe Frederick Jirenga, ameahidi kutekeleza maelekezo yote kwa usahihi na kwa wakati  na kushirikiana na watumishi ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wao.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals