[Latest Updates]: Waziri Mavunde Atatua Mgogoro wa Wachimbaji Madini Malera-Tarime

Tarehe : March 25, 2024, 9:14 a.m.
left

Aondoa zuio la awali la mgao wa mawe

Aelekeza Wachimbaji waruhusiwe na mgawo kuanzia kesho tarehe 26.03.2024

Wachimbaji waishukuru Serikali kwa utatuzi wa mgogoro na wenye Leseni za kuchimba dhahabu

Asisitza wachimbaji wadogo wasiondolewe katika maeneo ya uzalishaji

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde leo Machi 25, 2024  amefika katika eneo la Malera Wilaya ya Tarime, Mkoa wa Mara kwa ajili ya utatuzi wa mgogoro baina ya wachimbaji wadogo wamiliki wa Leseni na Kampuni ya KIRIBO ambao ulipelekea zuio la mgawo wa mawe mpaka baada ya utatuzi wa mgogoro huo.

Waziri Mavunde ametumia takribani saa 6 kutatua mgogoro husika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Mara, watendaji wa wizara na viongozi wa wachimbaji wadogo mkoa wa Mara (MAREMA)

“Ni maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan juu ya utatuzi wa migogoro mbalimbali katika sekta hii ya madini ambayo inadhoofisha kukua kwa uzalishaji wa madini," amesema Mavunde 

Aidha, amezipongeza  pande zote kwa kuridhia makubaliano katika hatua ya awali ya kutatua mgogoro huo.

Ameongeza kwamba kwa kuwa kulikuwa na zuio kwamba mgao wa mawe yaliyozalishwa usimame kwasababu ya mgogoro huu, ameelekeza  zuio hilo liondolewe na mgao wa mawe uanze kesho mapema tarehe 26.03.2024.

"Pia, hakikisheni katika utekelezaji wa wa maridhiano haya,  wachimbaji wadogo hawaondolewi katika eneo hilo na waachwe waendelee na shughuli zao," amesema Mavunde.

Akitoa maelezo ya awali, Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Said Mtanda amemshukuru Waziri Mavunde kwa kufanikisha utatuzi wa mgogoro husika na kupongeza hatua za kuruhusu mgao wa mawe kwa kuwa hali ya kipato ya wananchi wa eneo hilo ilikwenda chini na mapato ya serikali kutopatikana kwa wakati.

Zaidi ya watu 2000 wananufaika na mgodi huo ambao umekuwa ni shughuli kubwa ya kiuchumi ya wananchi wa Malera.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals