[Latest Updates]: Serikali kutoa Hati ya Makosa kwa wasioendeleza maeneo ya Madini

Tarehe : Aug. 10, 2018, 6:48 a.m.
left

Na Asteria Muhozya, Longido

Serikali imesema itatoa Hati za Makosa kwa wamiliki wa leseni za uchimbaji madini ambao hawajaendeleza maeneo yao na endapo hawatatii matakwa ya Sheria, watafutiwa leseni zao na maeneo  yao kupewa wombaji wengine.

Waziri wa Madini Angellah Kairuki ( kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (kulia) wakiangalia madini ya Ruby walipotembelea mgodi wa Mundarara Mine uliopo katika kijiji cha Mundarara , Wilaya ya Longido Mkoa wa Arusha, wakati wa ziara ya Waziri Kairuki katika machimbo hayo.[/caption]

Hayo yalielezwa na Waziri wa Madini Angellah Kairuki tarehe 9 Agosti, katika mkutano wa hadhara wakati wa ziara yake alipotembelea machimbo ya Ruby katika Kijiji cha Mundarara, Kata ya Mundarara, Wilaya ya Simanjiro mkoani Arusha.

Waziri Kairuki alitembelea migodi inayochimba madini ya Ruby katika eneo la Mundarara ili kuna namna shughuli za uchimbaji  wa madini hayo zinavyofanyika ikiwemo masuala ya afya na usalama migodini, kusikiliza changamoto na migogoro iliyopo katika machimbo hayo.

Alisema kuwa, Serikali inawajali wachimbaji wadogo nchini na kuwataka wenye nia ya kumiliki leseni za madini kufika katika ofisi za madini kwa ajili ya kupata taratibu za uombaji na  taratibu nyingine za umiliki wa leseni na kuongeza kuwa, bado serikali inaendelea kutenga maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo nchini.

Akizungumzia suala la utoaji ruzuku, Waziri Kairuki alimsema serikali inaangalia mfumo bora ambao inaweza kuutumia katika kuwasaidia wachimbaji wadogo nchini na kueleza kuwa, ruzuku hiyo inaweza kuwa katika mfumo wa  vifaa ama  namna nyingine.

Mwekezaji wa mgodi wa madini ya Ruby wa kampuni ya Mundarara Mine, akimwonesha Waziri wa Madini Angellah Kairuki Seal inayotumiwa mgodini hapo kufunga eneo yanapohifadhiwa madini ya Ruby baada ya uzalishaji.[/caption]

Pia, Waziri Kairuki aliwakumbusha wamiliki wa leseni za madini kuhakikisha wanajitambulisha katika ofisi za vijiji  mahali yalipo maeneo yao kabla ya kuanza shughuli za uchimbaji madini ili kutambuliwa  na uogozi wa kijiji  jambo ambalo litasaidia kuondoa migogoro.

Vilevile, Waziri Kairuki aliwataka wamiliki wa leseni za madini kuandaa Mpango wa Uwajibikaji kwa jamii na kueleza kuwa,  kwa mujibu wa sheria ya madini, mwekezaji anapaswa kushauriana na wananchi  wa eneo husika, chini ya usimamizi wa Halmashauri kuhusu maeneo ya uwajibikaji katika uwekezaji wake.

Pia, alizungumzia suala la Mpango wa kuwawezesha wananchi kiuchumi huku akisisitiza kuwa, endapo kuna shughuli ambazo zinaweza kufanywa na wananchi katika eneo husika, ni muhimu  jambo husika lifanyike hivyo.

Akitolea ufafanuzi suala la uongeaji thamani madini, alisema kuwa, serikali imekataza kusafirisha madini ghafi nje ya nchi ili yaongezewe thamani nchini na kueleza kuwa, tayari imeandaa mwongozo wa kutafsiri  dhana nzima ya uongezaji thamani madini na baada ya muda mfupi ujao itazungumzia kuhusu jambo hilo.

Waziri wa Madini Angellah Kairuki asalimiana na baadhi ya kina mama wa Kijiji cha Mundarara mara baada ya kuwasili katika kijiji hicho ili kuzungumza na wananchi. Wanaofuatilia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (katikati kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe.[/caption]

Waziri Kairuki alitoa ufafanuzi huo,  baada ya wawekezaji katika machimbo ya Ruby mundarara kuwasilisha ombi la kutaka madini hayo yasifirishwe yakiwa ghafi kutokana na aina ya madini yenyewe.

Pia, Waziri Kairuki alisema kuwa,Wizara kupitia Tume ya Madini itakuwa ikitoa bei elekezi za madini kila mwezi na kusimamia suala la uendeshaji wa minada ya madini nchini.

Aidh, masuala mengine aliyoyasisitiza Waziri Kairuki katika mkutano huo ni pamoja wachimbaji kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu. Wachimbaji kutunza kumbukumbu za uzalishaji na kuwa wazalendo kwa kutoa taarifa za wanaotorosha madini nje ya nchi

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akizungumza katika mkutano huo, alimtaka Waziri kupitia wizara yake kutoa ufafanuzi wa Sheria ya madini ili kuwawezesha wachimbaji kuitekeleza kwa mujibu wa kanuni na taratibu zake.

Pia, alimtaka Waziri wa Madini kusaidia kuweka mfumo mzuri wa biashara ya madini hayo na kuongeza kuwa, endapo kutawekwa mazingira mazuri ya biashara ya  madini hayo yatakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa eneo husika, wilaya na hatimaye taifa.

Afisa Madini akimwonesha Waziri wa Madini Angellah Kairuki maumbile ya miamba katika migodi yanapochimbwa madini ya Ruby katika eneo la Mundarara alipofika ili kusikiliza mgogoro uliopo baina ya wawekezaji wanaofanya shughuli za uchimbaji katika eneo hilo.[/caption]

Awali, akisoma risala ya kijiji, katika mkutano huo, Diwani wa Kata  Mundarara, Alais Mushao aliwasilisha changamoto ya soko la kuuzia madini ya ruby na kumuomba Waziri asaidie kuhakikisha kuwa, wawekezaji wadogo kupewa fursa sawa.

Katika mkutano huo, ziara hiyo aliongozana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, Mkuu wa Wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya , Wataalam kutoka Wizara ya Madini na Ofisi za Madini.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals