[Latest Updates]: Dkt. Biteko Auagiza Mgodi wa Almasi Mwadui Kukamilisha Tathmini Ajali ya Kubomoka kwa Bwawa la Tope

Tarehe : Nov. 10, 2022, 8:45 a.m.
left

DKT. BITEKO AUAGIZA MGODI WA ALMASI MWADUI KUKAMILISHA TATHMINI AJALI YA KUBOMOKA KWA BWAWA LA TOPE

#Mkuu wa Mkoa aunda Kamati kuchunguza chanzo, athari na kutoa mapendekezo

#Serikali kuchukua hatua kudhibiti madhara kutokea

Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko ameuagiza Mgodi wa Almasi wa Williamson Diamond Limited (WDL) kukamilisha tathmini ya ajali ya kubomoka kwa bwawa la tope na kuathiri sehemu ya makazi ya watu yanayozunguka eneo la mgodi.

Dkt. Biteko ametoa agizo hilo Novemba 10, 2022 akiwa katika eneo la Mgodi wa WDL wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kubaini athari zilizojitokeza baada ya bwawa la mgodi huo kubomoka Novemba 7, 2022 na kuleta athari kwa mgodi na jamii zinazozunguka mgodi.

Ameutaka mgodi huo kukamilisha kufanya tathmini ya wote waliopata madhara katika mashamba yao, mifugo na makazi ili walipwe fidia na mgodi huo.

Aidha, Dkt. Biteko ameutaka mgodi wa WDL kuharakisha kufanya tathmini ili shughuli za uzalishaji katika mgodi ziweze kuendelea katika muda uliopangwa.

Pia, amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwa kuunda Kamati maalum inayochunguza chanzo cha bwawa kubomoka, kutambua athari zilizojitokeza na kutoa mapendekezo kwa Serikali kuhusu tukio hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, ameahidi kutekeleza maagizo yote yaliyotolewa na Waziri wa Madini ikiwemo kusimamia Kamati iliyoundwa kufanya tathmini ili iweze kukamilisha kwa haraka.

Naye, Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo ameiomba Kamati iliyoundwa kuhakikisha inatenda haki katika mchakato mzima wa tathmini ili wananchi walioathirika wapate haki zao.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Mgodi wa WDL, Mhandisi Ayoub Mwenda, amesema hadi sasa watu 115 waliojitokeza kutokana na kuathiriwa na tukio wamehifadhiwa katika mazingira salama na kupatiwa huduma zote stahiki ikiwa ni pamoja na wanafunzi kupelekwa shuleni.

ReplyForward

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals