[Latest Updates]: Serikali Yatunga Kanuni Kuzuia Wageni Kuingia Kwenye Leseni Ndogo za Uchimbaji Madini Bila Utaratibu

Tarehe : April 27, 2025, 9:18 p.m.
left

Serikali kupitia Wizara ya Madini imetunga kanuni za msaada wa kiufundi katika Leseni ndogo za uchimbaji wa Madini ambapo zitaratibu ushiriki wa wageni katika Leseni ndogo za uchimbaji wa Madini(PML) ambazo kwa mujibu wa kifungu cha 8 cha Sheria ya Madini sura ya 123,kimezitamka Leseni hizi kama maalum kwa ajili ya Watanzania.

Kifungu cha 8(3) cha Sheria ya Madini kinatoa ruhusa kwa mmiliki wa Leseni ndogo ya uchimbaji madini kuingia ubia na mgeni kwa makubaliano ya msaada wa kiufundi(Technical Support).

Akiwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Madini kwa mwaka 2024/25 Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde alisema Serikali inatarajia kutunga kanuni za kuratibu ushiriki wa wageni katika Leseni ndogo kwa kuwa kumejitokea wimbi kubwa la wageni kuingia katika maeneo ya wachimbaji wadogo kwa mgongo wa “Msaada wa Kiufundi”ambao haukuwa na utaratibu mzuri na hivyo kupelekea wachimbaji wengi wadogo kutopata manufaa yaliyokusudiwa ya kujiimarisha kupitia Leseni ndogo za uchimbaji na wakati mwingine katika vikundi vya wachimbaji viongozi wachache kuingia makubaliano ya msaada wa kiufundi bila kushirikisha wahusika wote na hivyo kuzua migogoro isiyo na sababu.

Tarehe 25.04.2025 limetolewa Tangazo la Serikali Na. 260 kuitambulisha kanuni hii mpya kuanza utekelezaji wake ikiwa ni ahadi iliyotolewa na Waziri Mavunde akitekeleza maelekezo ya Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan.

Kanuni hiyo imetaja mambo mengi muhimu,yakiwemo;

1. Usajili wa Mikataba ya Kiufundi kwenye Tume ya Madini baina ya Mchimbaji Mdogo na Mtoa Msaada wa kiufundi.

2. ⁠Kufafanua maana ya maneno “Msaada wa Kiufundi” ili kutimiza lengo mahsusi la kuongeza tija ya uzalishaji na kukuza ujuzi.

3. ⁠Mgawanyo wa Mapato kati ya Mwenye Leseni Ndogo na Mtoa msaada wa Kiufundi kwa madini yatakayozalishwa.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals