Tarehe : March 26, 2025, 12:43 p.m.
Wizara Yabainisha Vipaumbele vya Mwaka 2025/26
Dodoma
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini leo Machi 26, 2025, imepitisha Maelezo ya Randama ya Wizara ya Madini kuhusu Makadirio ya Mapato , Matumizi ya Kawaida na Fedha za Maendeleo kwa Mwaka wa Fedha 2025/26, hatua inayotoa nafasi ya kuwasilishwa Bungeni.
‘’ Kamati imepitisha mapendekezo yenu kwa ajili ya hatua inayofuata, ninapenda kuwatakia utekelezaji mwema wa majukumu ya Wizara,’’ amesema Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt. David Mathayo akizungumza katika kikao hicho.
Katika kikao hicho, wajumbe wa kamati wamepata nafasi ya kuchangia, kutoa maoni, mapendekezo, ushauri na kupata majibu ya hoja walizotoa yote yakilenga kuendelea kuboresha na kuendeleza usimamizi wa rasilimali madini nchini.
Awali, akiwasilisha mapendekezo ya Wizara, Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango kutoka Wizara ya Madini Augustine Olal, ameieleza Kamati kuhusu majukumu mbalimbali yaliyotekelezwa na Wizara kwa Mwaka 2024/25 pamoja na kutoa taarifa kuhusu mipango na vipaumbele vilivyowekwa kutekelezwa kwa mwaka wa Fedha 2025/26.
Amevitaja vipaumbele hivyo kuwa ni pamoja na kuimarisha ukusanyaji wa maduhuli; kuongeza mchango wa sekta ya madini kwenye ukuaji wa Pato la Taifa; kuendeleza mnyororo wa thamani katika madini muhimu na madini mkakati;
Vipaumbele vingine ni pamoja na kuhamasisha uwekezaji na uongezaji thamani madini; kuimarisha uendeshaji wa minada na maonesho ya madini ya vito; kuongeza uwekezaji kwenye tafiti za madini za kina; kuwarasimisha na kuwaendeleza wachimbaji wadogo; na kuzijengea uwezo taasisi zilizo chini ya Wizara ya Madini.
Akitaja baadhi ya mafanikio, amesema uanzishwaji wa ndani wa minada ya vito ambapo jumla ya wanunuzi 47 walipatikana kama washindi wa mnada na kufanikiwa kununua madini kwa thamani ya shilingi 1,139,074,716.00 na Serikali ilifanikiwa kukusanya jumla ya shilingi 80,874,304.84 ikijumuisha mrabaha wa shilingi 68,344,482.96, ada ya ukaguzi ya shilingi 11,390,747.16 na ada ya usimamizi wa mnada ya shilingi 1,139,074.72.
Ameyataja mafanikio mengine kuwa ni pamoja na makusanyo ya jumla ya Shilingi 141,780,303,811.70 ikijumuisha shillingi 122,696,415,026.79 kutokana na malipo ya mrabaha na shilingi 19,083,888,784.91 kama ada ya ukaguzi kutokana na mauzo ya madini yenye thamani ya shilingi 2,169,443,670,358.36 kupitia masoko 43 ya madini na vituo vya ununuzi wa madini 109.
Naye, Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde akizungumza katika kikao hicho, ameieleza kamati kuhusu mikakati mbalimbali iliyopangwa kutekelezwa na Wizara ikiwemo masuala ya kufanya utafiti wa kina, uongezaji thamani hapa nchini, uendelezaji wachimbaji wadogo kwa kutungwa Kanuni na miongozo mbalimbali ya kuwawezesha kufanya shughuli zao vizuri kwa tija.
#InvestInTanzaniaMiningSector
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.