[Latest Updates]: ZIJUE DONDOO MUHIMU KUHUSU KIWANDA CHA KWANZA CHA KUCHENJUA SHABA KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA KISASA CHA MAST- CHUNYA MBEYA

Tarehe : June 19, 2025, 1:44 p.m.
left

KUANZISHWA
Mineral Access Systems Tanzania Ltd (MAST) ni Kampuni ya Kitanzania, iliyoanzishwa mwaka 2011, ikiwa na dhamira ya kuendeleza biashara ya madini kwa njia shirikishi na endelevu. Imekuwa ikifanya biashara ya madini ya kimkakati (strategic minerals) ndani na nje ya nchi mfano Zambia, Congo, Zimbabwe na South Africa, hususan shaba, nikeli na manganese, kwa kushirikiana na wachimbaji wadogo katika mikoa mbalimbali nchini.

UWEKEZAJI
Kiwanda cha MAST - Chunya ni matokeo ya uwekezaji wa zaidi ya dola milioni 10 za Kimarekani (USD) ikiwa ni uwekezaji wa ubia kati ya Kampuni ya MAST na MCC kutoka New York, Marekani.

LENGO LA KUANZISHWA
Kuchenjua madini ya shaba yenye kiwango cha chini 0.5 hadi asilimia 2 yanayopatikana katika eneo hilo la Mbugani Chunya na kuyapandisha thamani kufikia hadi asilimia 75 (copper cement) kwa kutumia teknolojia ya leaching na cementation.

UWEZO WA SASA WA UZALISHAJI
Kwasasa  kiwanda  kina uwezo wa kuchakata takriban tani 31,200 za mashapo ya shaba kwa mwezi, ambapo tani 27,200 zitatoka katika mgodi  wa kampuni hiyo ya MAST, na tani 4,000 zitanunuliwa kutoka kwa wachimbaji wadogo nchini.

MPANGO WA UJENZI WA VIWANDA VINGINE NCHINI
MAST ina mpango wa kujenga viwanda vingine vitatu vya uchenjuaji katika mikoa ya Manyara-Simanjiro, Ruvuma-Mbesa (Tunduru), na Dodoma, kila kimoja kikitarajiwa kutoa ajira zaidi ya 500 na kuchochea athari za kiuchumi zenye thamani ya USD milioni 40 kwa mwaka.

MPANGO WA UANZISHAJI MITAMBO MINGINE
Kiwanda kimejipanga kuanzisha mitambo maalum ya usindikaji wa nikeli kwa ajili ya kushughulikia aina zote mbili mbale za madini ya Nikeli ambazo ni laterite na sulfide. Hatua hii inalenga kutekeleza kwa vitendo dhamira ya kitaifa ya kuongeza thamani ya madini yote yanayochimbwa ndani ya mipaka ya nchi.

AJIRA ZILIZOZALISHWA HIVI SASA
Tayari kiwanda kimetoa ajira kwa wafanyakazi 254, wakiwemo 209 waajiriwa moja kwa moja wa MAST na 45 kupitia wakandarasi. Kati ya hao, watanzania 205 wamenufaika moja kwa moja ambao takriban ya asilimia 60 ya hao wakitoka Mkoa wa Mbeya, Wilaya ya Chunya.

MPANGO WA BAADAYE KUONGEZA AJIRA
Matarajio ya awamu inayofuata ni kuongeza ajira hadi zaidi ya 500, ambapo asilimia 95 ya wafanyakazi watakuwa Watanzania.

MAPATO KWA SERIKALI KUU NA HALMASHAURI
Kwa shehena ya kwanza pekee ya tani 200, jumla ya Shilingi milioni 228 zimeshalipwa kwa Serikali, na zaidi ya Shilingi milioni 9 kwa halmashauri ya wilaya ya Chunya.

UWAJIBIKAJI WA KAMPUNI KWA JAMII (CSR)
Mradi huu pia umeonesha mfano bora wa uwajibikaji kwa jamii (CSR), kwa kutoa vifaa vya michezo, kutengeneza barabara ya kijiji ya kilomita 6 na kujenga barabara mpya ya kilomita 11.


AZMA YA SERIKALI KUONGEZA THAMANI MADINI
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuendeleza viwanda vya kuongeza thamani ya madini nchini, kwa lengo la kukuza ajira, kuongeza mapato ya Serikali, na kuimarisha uchumi wa wananchi kupitia rasilimali za ndani.

IDADI YA LESENI ZA KUCHENJUA SHABA NCHINI
Hadi kufikia mwezi Mei, 2025  Wizara kupitia Tume ya Madini  imekwishatoa jumla ya Leseni Nne za kuchenjua Shaba miongoni mwake ni kiwanda cha MAST   Chunya. Leseni nyingine ni katika mikoa ya Dar es Salaam, Iringa na Lindi.


FURSA KUPITIA KIWANDA CHA MAST
Kiwanda cha MAST ni soko la uhakika kwa wachimbaji wadogo nchini. Fursa za kandarasi mbalimbali na utoaji huduma.

MIKOA YENYE MADINI YA SHABA CHINI
Tanzania imebarikiwa kuwa na shaba katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya Ziwa Victoria katika mikoa ya Geita, Mara, Shinyanga na Mwanza. Ukanda wa Magharibi – mikoa ya Katavi, Rukwa, Kigoma, Mbeya na Njombe na Ukanda wa Kusini mikoa ya Lindi na Ruvuma pamoja na ukanda wa  Kati  mikoa ya  Dodoma, Iringa na Morogoro. Duniani, kutokana na takwimu za mwaka 2023 kutoka taasisi ya jilojia na utafiti wa madini ya marekani (usgs) zinaonesha kuwa wazalishaji wakubwa wa shaba duniani ni Chile, Peru, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), China na Marekani na kwa upande wa Afrika ni nchi ya Zambia.

MATUMIZI YA SHABA
Shaba inatajwa kuwa moyo wa teknolojia za kisasa na kiungo muhimu katika mabadiliko ya nishati safi. Inaelezwa kwamba matumizi yake yamekuwa yakiendelea kadri dunia inavyoelekea kwenye nishati mbadala na inayohitajika katika karibu sekta zote za kiuchumi.  Mbali na matumizi mengine, hutumika kwenye magari ya umeme, mitambo ya upepo, panel za jua hadi kwenye nyaya za umeme wa majumbani na yanatajwa kuwa madini ambayo matumizi yake hayana ukomo.

CHUNYA KWA UJUMLA
Ni Mkoa wa pili wa Kimadini Kwa uzalishaji wa Madini ya dhahabu ikitanguliwa na Geita. Kufuatia kuanzishwa Kwa kiwanda Cha MAST, uchumi wa Chunya kupitia Sekta ya Madini unatarajiwa kukua kwa kasi.

 #UongezajithamaniMadiniNchini

#Value Addition

#MadininiMaishana Utajiri

#Madinini Uchumi

#MadininiAjira

#MadininiMaendeleo

#InvestInTanzaniaMiningSector

#Hii ndiyo Sektaya Madini.  10.1%mwaka mmoja kabla ya lengo

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals