Tarehe : March 23, 2022, 10:23 a.m.
# Agenda Kuu katika Mkutano wa Baraza hili ni kupitia na kujadili utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka 2021/2022 na kupitia makadirio ya Bajeti ya wizara kwa mwaka 2022/2023. Pia, wajumbe watapata nafasi ya kupitia taarifa ya mapato na matumizi ya Mwaka 2021/2022 na masuala ya kiutawala na utumishi ya mwaka 2021/2022.
# Katika kipindi hiki mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa umendelea kuimarika ambapo katika kipindi cha miezi tisa (Januari hadi Septemba 2021) mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la taifa uliongezeka hadi kufikia asilimia 7.3 kutoka mchango wa asilimia 6.5 katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2020.
# Katika robo ya Tatu Julai- Septemba 2021, Sekta ya Madini imechangia asilimia 7.9 ya Pato la Taifa, Mwelekeo unaonesha kuwa malengo yetu ya kuhakikisha sekta hii inachangia asilimia 10 ya Pato la Taifa ifikapo mwaka 2025 kama ilivyo matakwa ya Dira ya Taifa ya Maendeleo, 2025 na Mpango wa tatu wa Maendeleo ya Taifa yanatekelezeka kila mtu akitimiza wajibu wake.
# Katika kipindi cha kuanzia Julai 2021 hadi kufikia Februari 2022, tumefanikiwa kukusanya maduhuli ya shilingi bilioni 404.6, sawa na asilimia 62.6 ya lengo la makusanyo.
v Katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai 2021 hadi Februari 2022, wizara kupitia Tume yaMadini ilitoa jumla ya leseni 6,382 zikihusisha leseni za utafutaji wa madini, uchimbaji madogo, uchimbaji wa kati, uchimbaji mkubwa, uchenjuaji wa madini, usafishaji madini na biashara ya madini.
# Kupitia STAMICO imewezesha mafunzo na huduma mbalimbali kwa wachimbaji wadogo wapatao 1,144 waliotembelea vituo vya mfano vya Katente, Lwamgasa na Itumbi.
# Tumendelea kutangaza fursa zilizopo katika Sekta ya Madini kupitia mikutano ya kitaifa, kikanda na kimataifa ukiwemo mkutano wa kimataifa tulioandaa mwezi februari 2022.
# Tumeboresha Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali kwa lengo la kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji.
# Katika kuboresha ukusanyaji maduhuli, wizara imeanzisha mfumo wa kukusanya maduhuli ya madini ujenzi katika Mikoa ya Dar es salaam, Morogoro na Dodoma na unatarajiwa kutumika nchi nzima.
# Pamoja na mafanikio niliyoyataja, wizara inakabiliwa na changamoto za uwepo wa shughuli za utoroshaji wa madini zinazosababisha upotevu wa mapato ya serikali, uelewa mdogo wa wachimbaji, wafanya biashara wa madini na umma kwa ujumla kuhusu Sheria ya madini, hivyo kusababisha uwepo wa migogoro ya mara kwa mara.
# Ili kukabiliana na changamoto hizo, wizara imeweka mikakati na hatua mbalimbali ya kukabiliana nazo ikiwemo; kuimarisha usimamizi wa shughuli za madini na ukusanyaji wa mapato ya serikali yatokanayo na wasilimali madini kwa kushirikisha mamlaka mbalimbali.
# Wizara imeendelea kutoa elimu na mafunzo ya mara kwa mara kwa wadau mbalimbali katika maeneo ya wachimbaji wadogo pamoja na viongozi wa Serikali za Mitaa kwa kuwajengea uelewa kuhusu dhana nzima ya kufuata Sheria ya Madini na Kanuni zake ili kuepuka migogoro.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.