[Latest Updates]: Kiwanda cha Kuchenjua Madini ya Shaba Mbioni Kuanzishwa Tunduru

Tarehe : Aug. 16, 2022, 5:04 p.m.
left

Kiwanda cha kuchenjua Madini ya Shaba kinatarajiwa  kuanzishwa wilayani Tunduru Mkoa wa Ruvuma ili kuwezesha shughuli za kuchenjua madini hayo kufanyika nchini na hivyo kulinufaisha taifa na watanzania.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko leo Agosti 16, 2022 mkoani Mwanza alipokutana na Kampuni ya Mineral Access System Tanzania Limited inayotarajia kujenga  kiwanda cha kuchenjua madini ya Shaba katika eneo la Mbesa wilayani Tunduru.

Dkt. Biteko, amewapongeza kuwekeza nchini kwani uwepo wake utasaidia kuongeza thamani ya madini na hivyo kuongeza tija ya kiuchumi kwa taifa na kwa wanachi wa Tunduru.

Amesema, Serikali itaendelea kuvutia wawekezaji  ili kuwekeza katika Sekta ya Madini kwa kuwa tayari imeweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji kwenye mnyororo wote wa shughuli za madini ikiwemo shughuli za utafiti, uchimbaji na uongezaji thamani madini nchini bila changamoto yoyote.

"Serikali kupitia Wizara ya Madini itaendelea kuvutia wawekezaji kuja kuwekeza katika Sekta ya Madini ili Watanzania wanufaike na rasilimali hiyo," amesema Dkt. Biteko.

Vile vile, Dkt. Biteko amesema Serikali itahakikisha inaweka mazingira wezeshi ili kutatua changamoto ya ucheleweshwaji wa mizigo kuingia nchini kutokana na taratibu za forodha. Aidha amesisitiza  kuwasilisha changamoto hiyo katika mamlaka husika.

Kwa upande wake, Rais na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Metallica Commodities Corp, Glendon Archer amesema kiwanda hicho  kitawezesha kuboresha maisha ya wananchi katika maeneo hayo na kuongeza Pato la Taifa.

Pia, ameahidi kushirikiana na Serikali katika kipindi chote cha uzalishaji ili manufaa ya kiwanda hicho yabaki nchini. 

Archer amemshukuru Dkt. Biteko kwa ushirikiano anaopatiwa na Wizara ya Madini katika kila hatua ili kuweza kujenga kiwanda hicho na kuanza uzalishaji.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kusini, Mhe. Daimu Mpakate, amesema kiwanda hicho kitaongeza fursa mbalimbali kwa wananchi na Serikali. 

Ameongeza kuwa, wawekezaji hao wa madini ya Shaba watatoa ajira na kuboresha miundombinu ya maeneo hayo hususan kwa wakazi wa Tunduru.

Kampuni ya Mineral Access System Tanzania Limited pia inatarajiwa kuwekeza kwenye madini ya Lithium na Nikeli nchini.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals