[Latest Updates]: Mkutano wa Kimataifa Uwekezaji Sekta ya Madini Kutangaza Fursa ya Madini Mkakati Tanzania

Tarehe : Oct. 24, 2023, 5:16 p.m.
left

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amesema Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 na 26 jijini Dar es Salaam utatangaza fursa ya Madini Mkakati na Muhimu yaliyopo hapa nchini.

Ameyasema hayo leo Oktoba 24, 2023 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza katika kipindi cha runinga cha Jambo Tanzania kinachorushwa na kituo cha Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC 1).

Amesema kuwa mwekekeo wa Dunia kwa sasa ni kuhamia katika matumizi ya nishati safi na kupunguza matumizi ya nishati inayochafua mazingira na kwamba Tanzania itashiriki kikamilifu katika uchumi huo wa Madini Mkakati ili kuongeza zaidi mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa na uchumi kwa ujumla. 

“Mwenyezi Mungu ametujaalia kuwa na Madini Mkakati kama vile Shaba, Lithiamu, Nikeli, Kobalti na Vipengele Adimu vya Dunia (REE) ambayo ni  muhimu katika teknolojia nyingi za nishati safi zinazoendelea kukua kwa kasi kwa ajili magari ya umeme” amesema Mhe. Mavunde. 

Mhe. Mavunde amesema mkutano huo, utaiweka Tanzania katika ramani ya uchumi duniani, kwa kuwa ni fursa ya kipekee ya kutangaza madini yalipo na kuwavutia wawekezaji. 

Ameongeza kuwa, Mkutano huo utasaidia kubadilishana uzoefu pamoja na teknolojia na mataifa yaliyofanikiwa zaidi kiuwekezaji katika eneo la rasilimali Madini.

VISION 2030: Madini ni Maisha na Utajiri.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals