Tarehe : March 11, 2026, 1:05 p.m.
- Ahaidi kushirikiana na wadau wote wa TEITI
- Suala la utekelezaji wa shughuli za EITI nchini ni shirikishi
- Ashukuru Mgodi kwa kutekeleza takwa la CSR
- Apongeza Mchango wa Mgodi katika Mapato ya Serikali
Geita.
Leo tarehe 11 Machi, 2026 Mwenyekiti wa Kamati ya TEITI Balozi Wilson Masilingi akiambatana na Menejimenti ya TEITI watembelea Mgodi wa Dhahabu wa GEITA.
Lengo la ziara hiyo ni kujitambulisha kwa Menejimenti ya Mgodi ili kufahamiana kwa kuwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hasan mwezi Januari aliniteua kusimamia Taasisi hii Muhimu kwa maendeleo ya sekta ya Uziduaji hapa nchini alisema Balozi Masilingi.
Katika ziara ilikuwa fursa ya kujifunza maendeleo yaliyofanywa na Mgodi tangu ulipoanzishwa ambapo ilielezwa kuwa Mgodi umeendeleaje kusimamia Sheria na miongozo iliyowekwa ikiwemo masharti ya leseni iliyotolewa kwa ajili ya uchimbaji wa rasilimali madini hapa nchini.
Aidha, ilielezwa kuwa Mgodi umekuwa ukitenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya CSR katika Halmashauri zilizopo katika Mkoa wa Geita.
Ilielezwa kuwa kwa sasa Mgodi unaendeshwa na Watanzania kwa Asilimia kubwa na kuajili watanzania wengi kuliko ilivyokuwa hapo awali.
Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa TEITI Bi. Mariam Mgaya ameishukuru menejimenti ya Mgodi kwa kuendelea kushirikiana na TEITI katika utekelezaji wa matakwa ya EITI pamoja na Sheria ya TEITA, 2015 inayosimamia masuala la uwazi na uwajibikaji katika sekta ya uziduaji.
Pia, alisisitiza ushirikiano huu uendelee ili kuongeza uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia.
Balozi Masilingi ameushukuru Mgodi wa Dhahabu wa Geita kwa mapokezi mazuri ambayo yaneonesha mwanga wa mashirikiano zaidi kwa siku za usoni, alisisitiza Balozi Masilingi. Nitashirikiana na wadau wote wa TEITI kikamilifu ili uendelea gurudumu ya uwazi na uwajibikaji katika sekta ya uziduaji hapa nchini.
Meneja wa Mgodi wa Geita Bw. Ashraf Suryaningrat amehaidi kushirikiana na TEITI kikamilifu ili kufikia lengo la uwazishaji wake kwa kuwa Mgodi wa Geita ni wadau wakubwa wa TEITI.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.