Tarehe : Nov. 26, 2025, 12:28 p.m.
Leo tarehe 26, Novemba 2025 – Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), lilipata wasaa wa kuupokea Ujumbe kutoka Zambia katika mradi wake wa ubia wa Mwanza Precious Metals Refinery( MPMR) uliopo jjini Mwanza.
Ujumbe huo ambao uliongozwa na Balozi wa Zambia nchini Tanzania, Mhe. Matheus Jere ambaye aliambatana na wawakilishi kutoka Wizara ya Madini kwa lengo la kujifunza kuhusu namna STAMICO inavyoendesha shughuli zake pamoja na usimamizi wa miradi yake.
Akizungumza katika wasilisho fupi, Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance B. Mwasse, alieleza namna Shirika linavyojiendesha kupitia miradi yake ikiwemo mradi mkubwa wa kutoa huduma ya uchorongaji pamoja na manufaa yanayopatikana kwa Shirika kuwekeza kwa niaba ya umma. Katika ziara hiyo, Dkt. Venance Mwasse aliambatana na Bw. Deusdedith Magala, Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala ambaye pia ni Katibu wa kiwanda cha MPMR.
Kwa upande wake, Mhe. Balozi Matheus Jere alionesha kufurahishwa na namna Shirika linavyofanya kazi na kutoa pongezi kwa STAMICO na kiwanda cha MPMR.
Vilevile, Mhe. Balozi ametoa rai kuwepo na Makubaliano ya Ushirikiano (MOU) kati ya STAMICO na ZCCM (Zambia Consolidated Copper Mines Ltd) hususan katika maeneo ya kubadilishana uzoefu.
Utendaji bora wa STAMICO umeendelea kuwavuta mataifa mbalimbali kuja kujifunza namna Serikali inavyoweza kusimamia na kushiriki katika uvunaji wa rasilimali madini kwa manufaa ya taifa lake.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.