Tarehe : Oct. 1, 2018, 7:52 a.m.
Na Nuru Mwasampeta, Dodoma
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki leo tarehe 28 Septemba, 2018, amefanya mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo Nchini (FEMATA), John Bina ambaye aliambatana na Mtendaji Mkuu wa Shirikisho hilo, Bwana Haroun Kinega, ofisini kwake jijini Dodoma.
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Shirikisho la Wachimbaji Wadogo wa Madini John W. Bina (Kulia) na kushoto kwa waziri ni Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Wachimbaji wadogo Haroun[/caption]
Katika kikao hicho, Waziri Kairuki amewashukuru wajumbe hao kwa kumtembelea ofisini kwake na kujadiliana masuala mbalimbali katika sekta ya madini kwa lengo la kuboresha utendaji katika sekta ya madini, uchimbaji na wachimbaji wadogo kwa ujumla.
Aidha, Waziri Kairuki amewataka watanzania wenye mawazo chanya ya kukuza sekta ya madini kutosita kufika na kutoa maoni yao ili Serikali iweze kuyafanyia kazi ili kuboresha sekta hiyo kwa manufaa ya jamii nzima ya watanzania na hivyo kuifanya sekta kuchangia zaidi katika pato la taifa, ajira na kukuza uchumi wa nchi.
Akizungumzia lengo la kufika wizarani hapo, Rais wa FEMATA, John Bina amesema ni kujadili kuhusu mafanikio, changamoto, fursa za wachimbaji wadogo zilizopo katika sekta husika pamoja na kujadili namna ya kuendeleza sekta ya uchimbaji mdogo wa madini nchini ikiwa ni pamoja na namna ya kudhibiti utoroshaji wa madini nchini.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.