Tarehe : Nov. 26, 2025, 12:32 p.m.
Bodi ya Wakurugenzi ya BOT, ikiongozwa na Bw. Emmanuel M. Tutuba, Gavana na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, imetembelea kiwanda cha Mwanza Precious Metal Refinety (MPMR) kwa lengo la kuongeza uelewa katika shughuli za kiwanda na kujionea mafanikio ya pamoja na maendeleo ya kiwanda kiujumla.
Kwa upande wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), liliwakilishwa na Dkt. Venance B. Mwasse, Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO ambaye aliongozana na Bw. Deusdedith Magala, Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala ambaye pia ni Katibu wa kiwanda cha MPMR.
Katika ziara hiyo, Dkt. Venance B. Mwasse alieleza chimbuko la mradi wa MPMR pamoja na manufaa yaliyopatikana ambayo ni pamoja na kuiwezesha BOT kufikia malengo yake ya kununua dhahabu.
Kufuatia kukamilika ziara na wasilisho, Gavana kwa niaba ya Bodi aliridhishwa na kazi inayoendelea kiwandani hapo na alitoa pongezi kwa STAMICO pamoja na uongozi wa MPMR kwa kazi nzuri inayofanyika.
Pia Gavana ametoa rai kwa kiwanda cha MPMR kuongeza jitihada za kupata ithibati ya LBMA pamoja na kuongeza mikakati zaidi ya kupata malighafi, ikiwemo kuwawezesha wachimbaji wadogo kifedha
Awali Bodii ya Ushauri ya Chuo cha Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ilitembelea kiwanda hicho.
Bodi ya Ushauri ya Chuo cha BOT iliambatana na Makamu Mkuu wa Chuo Dkt. Ephraim Mwasanguti kwa lengo la kujifunza na kujionea jinsi kiwanda kinavyoendesha shughuli zake za uongezaji thamani wa madini ya dhahabu pamoja na fedha kwa viwango vya kimataifa.
Bodi ilifurahishwa na ziara hiyo kwa kuwa imekuwa na manufaa sana na wameweza kujifunza na kutoa pongezi kwa kiwanda cha MPMR kwa mafunzo na mapokezi waliyoyapata.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.