[Latest Updates]: Biteko - Nitasimama na Mzee Kisangani mpaka “asimame”

Tarehe : March 15, 2020, 9:56 a.m.
left

Na Issa Mtuwa – Ludewa

Waziri wa Madini Doto Biteko amesema kumekuwa na kasumba ya kuwathamini wageni kutoka nje ya nchi kuliko wazawa wenye ubunifu na uthubutu katika kazi zao, wakati wageni kutoka nje wanakuja na mtaji mdogo na mwisho wa siku huondoka na utajiri mkubwa.

Yamesemwa hayo leo tarehe 14 Machi, 2020 akiwa ziarani mkoani Njombe alipotembelea mradi wa kiwanda cha kuzalisha zana mbalimbali zinazotokana na madini ya chuma kinachomilikiwa na Reuben Mtitu maarufu Mzee Kisangani

Biteko alishangazwa na ubunifu na uthubutu wa Mzee Kisangani namna hatua aliyofikia huku akisema endapo mzee huyu angekuwa “mweupe” watu wangeenda na lugha mbalimbali na kuhangaika nae lakini kwa kuwa yeye ndio kama sisi, watu hasa wa serikali bado hawajamhangaikia.

Amesema kutokana na ubunifu aliouonyesha hakika atasimama nae mpaka “asimame”. Ameongeza kuwa ubunifu na uthubutu wake pamoja na kukosa mtaji na ukosefu wa mambo kadhaa ya kisheria wizara yake itamsaidia mzee huyo kuhakikisha kiwanda chake kinakuwa kikubwa hadi ya kuzalisha bidhaa na kuwauzia watu wa maduka makubwa ya jumla.

“Nimefurahi sana kufika hapa, ubunifu na uthubutu wa mzee Kisangani unanipa nguvu ya kumsaidia.. Huyu mzee angalieni alianza na kutengeneza umeme wa kiholela, katengeneza kiwanda kwa ubunifu, watu 30 wapo kwenye kiwanda hicho na mpaka sasa ameshaanza utengenezaji wa Visu zaidi ya 10,000, Mapanga, 5,000, Fyekeo zaidi 2,000 na Majembe kutokana na uwepo wa madini ya chuma sisi wizara ya madini tutamsaidia”  emesema Biteko.

Nitawaomba “NDC” watenge eneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo. Wa madini ya Chuma, pia nitawaomba Wizara ya Viwanda na Biashara, Watu wa Mazingira  na Wizara ya Ardhi kuona ni namna gani tuweze kumsaidia huyu mzee hadi kufikia mahali hapa kuwe na kiwanda kikubwa.

Mzee Kisangani amemwambia Biteko kuwa uzalishaji wake wa bidhaa unatokana na baadhi ya changamoto mbalimbali hasa katika upatikanaji wa makaa ya mawe ya kuyeyusha chuma ili atengeneze bidhaa kwa kuwa makaa ya mawe anayoyatumia ni ya kuokota barabarani yanayodondoka kwenye magari yanayosafirisha makaa hayo kutoka Liganga.

Amesema bado kiwanda chake bado ni kidogo kutokana na teknolojia anayoitumia hivyo serikali imtazame na kumsaidia ili awe na kiwanda kikubwa na bora.

Ameongeza kuwa, hata umeme wa awali ni wa kubuni na kutokana na hali hiyo alipelekewa nguzo za umeme na REA ili apate umeme wa uhakika kwa ajili ya kazi zake japo bado umeme huo bado haujaletwa. Amesema, endapo changamoto zinazo mkabili angeweza kuwa na wafanyakazi wengi zadi ya hao 30 waliopo.

Kutokana na changamoto hizo, Biteko amesema ataongea na TANCOAL waweze kumsaidia mzee huyo kumshushi Lori mbili kwa mwezi Makaa ya Mawe ili aongeze uzalishaji.

Biteko amesema amemuagiza mzee huyo kupanua eneo la kiwanda hicho na kupaboresha. Alichokiona mahali hapo atamrejeshea ujumbe huo Waziri Mkuu alie mtaka Waziri kuja kumtembelea mzee huyo siku akifunga mkutano mkuu wa sekta ya madini siku ya tarehe 23 Februari, 2020.

Ameongeza kuwa, mbuyu huanza kama mchicha sio kushangaza badae mchicha huo ukawa mbuyu kama wanavyo simulia watu kuhusu chanzo cha utajiri wao.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals