Tarehe : May 26, 2025, 2:12 p.m.
Chaboresha miundombinu ya shule, barabara, maji na afya
Mtwara
Wananchi wa vijiji vya Likonde, Hiyari, Mkwajuni, Mwembetoga, Kyoba, Msijute, Mbuo na Mayanga, mkoani Mtwara, wameeleza kuridhishwa kwao na mchango mkubwa unaotolewa na Kiwanda cha Saruji cha Dangote katika kuboresha huduma za kijamii kwenye maeneo yao, hususan kwenye sekta za elimu, afya, maji na miundombinu ya barabara.
Akizungumza kwa niaba ya walimu na wakazi wa Kijiji cha Kyoba, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kyoba, Muksin Mnakane, amesema kuwa ujenzi wa shule mpya na nyumba za walimu, uliofanywa na kampuni hiyo, umeleta mageuzi makubwa katika utoaji wa elimu kijijini hapo.
“Awali wanafunzi walilazimika kutembea umbali wa zaidi ya kilomita mbili kwenda shule za vijiji vya jirani. Hali hiyo ilikuwa inachangia utoro na kushuka kwa ufaulu. Lakini sasa, kwa msaada wa kiwanda cha Dangote, watoto wanasoma karibu na makazi yao, na ufaulu umeimarika,” amesema Mnakane.
Ameongeza kuwa kiwanda hicho pia kimeboresha miundombinu ya barabara, jambo lililosaidia kupunguza ajali na kuwezesha wananchi kusafiri kwa urahisi hasa kipindi cha mvua.
“Walimu sasa hawatembei umbali mrefu kufika shuleni. Nyumba walizojengewa zipo karibu kabisa na shule, hivyo wanatimiza majukumu yao kwa wakati na kwa ufanisi zaidi,” ameongeza Mnakane.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi wa Miradi kutoka jamii, Bi. Tatu Salawanda, ameeleza kuwa kiwanda cha Dangote kimefanikiwa kujenga shule katika Kijiji cha Hiyari, nyumba za wahudumu wa afya katika vijiji vya Likonde na Mbuo, pamoja na barabara inayounganisha Kijiji cha Msijute na Zahanati ya Mayanga.
“Wananchi sasa wanaweza kufika hospitali kwa haraka. Aidha, ujenzi wa visima katika kijiji cha Majengo ambapo umesaidia sana wananchi kupata maji safi karibu na makazi yao, tofauti na awali walipolazimika kutembea umbali mrefu,” amesema Salawanda.
Naye Meneja wa Mahusiano wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote, Bw. Abeid Muda, amesema kuwa miradi hiyo ni sehemu ya mpango wa kampuni hiyo wa uwajibikaji kwa jamii (CSR) kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi wanaoishi karibu na kiwanda hicho.
“Mchango wetu unalenga kuleta maendeleo ya kweli kwa jamii. Tumejenga shule, nyumba za watumishi, barabara na miradi ya maji yote haya yakilenga kuwawezesha wananchi wa maeneo haya kufikia huduma bora kwa urahisi,” amesema Muda.
Kwa ujumla, juhudi za Kiwanda cha Dangote zinaendelea kuwa mfano wa kuigwa wa ushirikiano kati ya sekta binafsi na jamii katika kuleta maendeleo endelevu.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.