[Latest Updates]: Dkt. Kiruswa Aiagiza GST na STAMICO Kufanya Tafiti za Madini Mufindi na Kilombero

Tarehe : Sept. 20, 2022, 2:58 p.m.
left

Dodoma

Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) pamoja na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kufanya tafiti za madini katika wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro na wilaya ya Mufindi mkoani Njombe kwa lengo la kubaini aina ya madini yaliyopo katika wilaya hizo.

Hayo yamebainishwa na Dkt. Kiruswa wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Jimbo la Kilombero Abubakari Asenga katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni jijini Dodoma.

Aidha, Dkt. Kiruswa ameainisha maeneo mbalimbali yenye madini ya dhahabu na vito katika wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro.

Akijibu swali hilo amesema, Taasisi ya GST imefanya utafiti wa awali sambamba na kuchora ramani kwenye maeneo yote yaliyopo katika Jimbo la Kilombero katika mfumo wa Quarter Degree Sheet (QDS).

Dkt. Kiruswa amesisitiza kuwa, tafiti za awali zilizofanyika  katika wilaya ya Kilombero, zilionesha uwepo wa madini ya dhahabu na madini ya vito katika Kata ya Chisano.

Ameongeza kuwa, GST ilifanya utafiti wa awali na kuchora ramani ya eneo la Hifadhi ya Milima Udzungwa na maeneo jirani ambapo utafiti wa madini uliofanyika katika maeneo hayo hauoneshi taarifa zozote za uwepo wa madini ya thamani katika milima hiyo.

Mkoa wa Morogoro umebarikiwa kuwa na aina mbalimbali za madini ikiwemo dhahabu, Shaba, Kinywe, madini ya viwandani (Ulanga, Kaoline),  madini ya ujenzi (mchanga, kifusi) na madini ya vito ( Rubi, Rodolite).

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals