[Latest Updates]: Wizara ya Madini Kurusha Ndege ya Utafiti Geita

Tarehe : Sept. 26, 2023, 7:55 a.m.
left

• Kuongeza taarifa za utafiti wa kina

• Lengo ni kutoka 16%  kufikia 100%

Kutokana Wizara ya Madini kutambua mchango wa wachimbaji wadogo wa madini katika pato la Taifa, hivyo ipo na mkakati wa kufanya utafiti wa kina kwa kurusha ndege maeneo mbalimbali ikiwemo Geita   ili kupata taarifa sahihi za uwepo wa madini katika maeneo husika.

Hayo yamebainishwa Septemba 25, 2023 na  Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde wakati akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini mkoani Geita katika kongamano la kuibua fursa za madini pamoja na kujadiliana juu ya changamoto zinazowakabili wachimbaji wado

Mhe. Mavunde aliongeza kuwa Wizara ya Madini ipo katika mkakati wa kuongeza taarifa za utafiti wa kina wa madini kwa lengo la kufungamanisha sekta ya madini na sekta nyingine za kiuchumi .

Akifafanua kuhusu hali ya utafiti nchini Mhe. Mavunde alisema kuwa kwasasa Serikali imefanya utafiti wa kina kwa asilimia 16 ya eneo la nchi  ambayo taarifa zake  ndizo zinazotumika  kuendeleza  miradi ya uchimbaji madini.

Vilevile , Mhe.Mavunde aliongeza kuwa kutokana na umuhimu wa taarifa hizo Serikali imepanga ifikapo mwaka 2030 iwe imefanya utafiti wa kina nchi nzima ili kubaini  maeneo yote yenye rasilimali madini , hii itasaidia kuongeza wigo kwa wachimbaji wadogo ,wakati na wakubwa tofauti na ilivyo sasa.

Akielezea kuhusu mchango wa sekta ya madini katika pato la Taifa , Mhe. Mavunde alisema sekta ya Madini inaendelea kupaa na  mpaka sasa inachangia kiasi cha  asilimia 9.1, hii ni kwa taarifa za utafiti wa asilimia 16 tu, hivyo kwa kuongeza taarifa za kina sekta ya Madini itakuwa kinara katika uchangiaji katika sekta ya madini.

Awali , katika Kongamano hilo Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Madini ziliwasilisha mada mbalimbali juu ya mnyororo mzima wa sekta ya Madini ikiwa pamoja na mpango wa kuwainua wachimbaji wadogo ili wafanye uchimbaji wenye tija na uhakika.

Kongamano hilo lilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa Geita, Mbunge wa Geita Mjini,Taasisi za Fedha , Wakuu wa Taasisi za Umma na viongozi wa Vyama vya  Wachimbaji wadogo.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals