[Latest Updates]: Tanzania Yajipanga Kuzalisha Bidhaa Zitokanazo na Madini Nchini

Tarehe : Nov. 21, 2025, 1:42 p.m.
left

Ni maelekezo ya Mhe.Rais Samia ya uongezaji thamani madini nchini

Waziri Mavunde akagua ujenzi wa kiwanda cha kusindika na kuyeyusha madini ya Nikeli na Shaba

Kiwanda kuanza uzalishaji Februari,2026

Wachimbaji wadogo wapata soko la uhakika wa kuuza malighafi kiwandani

Mradi kugharimu Bilioni 37

Dodoma

Tanzania yaendelea kupiga hatua katika Mpango wa ujenzi wa viwanda vya uongezaji thamani madini kutokana na ujenzi wa kiwanda kipya cha usindikaji  na uyeyushaji madini ya Nikeli na Shaba kufikia asilimia 85 ya ujenzi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Mhe.Rais .Dkt.Samia Suluhu Hassan yanayoelekeza kuwa shughuli za uongezaji thamani madini kufanyika ndani ya nchi kabla ya kusafirishwa nje.

Hayo yameelezwa leo Novemba 21, 2025 na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde wakati anakagua kiwanda cha kusindika  na kuyeyusha madini ya Nikeli na Shaba kilichopo eneo la Mayamaya , Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma.

Mhe.Mavunde amesema kuwa, kiwanda kitawasha mtambo wake wa kwanza wa uzalishaji ifikapo mwezi Februari, 2026 ambapo mtambo huo utachakata tani 300 za mashapo kwa siku.

Akielezea kuhusu gharama za uwekezaji katika kiwanda hicho, Mhe. Mavunde amesema kuwa uwekezaji huu ni mkubwa utakapo kamilika utagharimu shilingi bilioni 37, hivyo amewataka wachimbaji wadogo wa madini nchini  kutumia fursa hiyo ya soko la uhakika  kupeleka malighafi katika kiwanda. 

Akifafanua kuhusu malengo ya kujenga viwanda vya uchakataji na uongezaji thamani madini , Mhe.Mavunde amefafanua kuwa shabaha kubwa ni kuhakikisha Tanzania inakamilisha mnyororo wote wa thamani madini kuanzia uchimbaji mpaka uchakataji na uongezaji thamani ili kusafirisha nje ya nchi  bidhaa zitokanazo na rasilimali madini badala kusafirisha  madini ghafi  kama ilivyokuwa awali.

Kwa upande wake,  Mkuu wa Wilaya ya  Bahi Mhe. Joachimu Nyingo amesema kuwa,  anaipongeza Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kupeleka wawekezaji wa madini mkoani Dodoma, jambo linalopelekea kufikia viwanda 9 vya uongezaji thamani madini.

Naye , msimamizi wa kiwanda hicho Hassan Ngaiza ameeleza juu ya faida mbambali za kiuchumi na kijamii zitaletwa na kiwanda hicho ikiwa pamoja na ajira zaidi ya 300 ambazo za kudumu na zisizo za kudumu, masoko  ya malighafi madini pamoja  na bidhaa nyingine.

Pamoja na mambo mengine, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wachimbaji Wadogo wa Madini ya Metali Tanzania Thobias Kente, ameushukuru uongozi wa kiwanda cha Zhong Zhou kwa juhudi kubwa inayofanya kuhakikisha kuwa  kiwanda kinakamilika kwa wakati, jambo ambalo litawezesha wachimbaji wadogo wa madini ya metali kupata soko la uhakika la madini ghafi wanayochimba nchini.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals