[Latest Updates]: Serikali Imeweka Kipaumbele Mradi wa Uchimbaji Dhahabu Nyanzaga - Katibu Mkuu Mahimbali

Tarehe : April 19, 2024, 4:39 p.m.
left

Asema Rais. Samia anafuatilia maendeleo ya Mradi huo kwa karibu.

Katibu Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali, amekutana na kuzungumza na Ujumbe wa Kampuni ya Perseus kutoka nchini Australia ukiongozwa na Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Bw. Jaffer Quartamaine.

Mazungumzo hayo yamefanyika baada ya Ujumbe huo kukutana na Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde Ofisini kwake Jijini Dodoma leo Aprili 19, 2024 na kujadili kuhusu uanzishwaji wa Mradi huo.

Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Wizara zilizopo Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma ambapo wamejadili kuhusu umuhimu wa Mradi wa Uchimbaji Madini ya Dhahabu wa Sotta uliopo Wilaya ya Sengerema, Mkoani Mwanza.

Katibu Mkuu Mahimbali ameueleza Ujumbe huo kuhusu matamanio ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuona Mradi huo unatekelezwa kwa wakati na kwamba anafuatilia kwa karibu maendeleo ya Mradi huo.

Aidha, Mahimbali ameongeza kuwa, Wizara ya Madini itaendelea kutoa kipaumbele na kusaidia Miradi yote iliyopo katika Sekta ya Madini ikiwemo Mradi huo kwa kuipa umuhimu mkubwa na kutatua changamoto zinazowakabili.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo ya Perseus Bw. Jaffer Quartamaine amesema kuwa Kampuni hiyo imefarijika kuona Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Madini imeupa umuhimu mkubwa Mradi huo wa Uchimbaji wa Madini ya Dhahabu na hivyo kurahisisha mchakato wa mradi katika kutekeleza majukumu yake.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals