Tarehe : Feb. 8, 2026, 10:36 a.m.
Waziri Mavunde Atoa Uzoefu Ushirikiano kati ya Sekta ya Nishati na Madini Tanzania
Aangazia Mradi wa Bwawa la Julius Nyerere, Upanuzi wa Gridi na Miradi ya REA
Cape Town – Afrika Kusini
Mawaziri wa Madini kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wameazimia kwa kauli moja kuweka mikakati madhubuti ya kuongeza thamani ya madini ndani ya nchi zao, hususan madini mkakati, ili kuongeza mapato ya taifa, kukuza uchumi na kuzalisha ajira. Katika azma hiyo, Sekta ya Nishati imetajwa kuwa nguzo muhimu katika kufanikisha utekelezaji wa mkakati huo.
Akizungumza katika mahojiano maalum baada ya kushiriki kikao cha Mawaziri kilichofanyika Februari 8, 2026, katika Kongamano la Mining Indaba jijini Cape Town, Waziri wa Madini wa Tanzania, Mhe. Anthony Mavunde, amesema kuwa ametumia jukwaa hilo kutoa uzoefu wa Tanzania kuhusu namna Sekta za Nishati na Madini zinavyoshirikiana kwa vitendo katika kutekeleza agenda ya uongezaji thamani wa madini kwa manufaa ya watanzania.
Waziri Mavunde ameeleza kuwa Serikali ya Tanzania imechukua hatua mbalimbali kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika ili kuimarisha shughuli za madini, ikiwemo uongezaji thamani madini na uchenjuaji madini. Miongoni mwa miradi mikubwa aliyoitaja ni mradi wa bwawa la kuzalisha nishati ya umeme la Julius Nyerere unaotarajiwa kuzalisha megawati 2,115 za umeme.
Aidha, Waziri Mavunde ameeleza kuhusu utekelezaji wa miradi ya usambazaji umeme vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), inayolenga kufikisha umeme katika maeneo yenye shughuli za madini ili kuongeza uzalishaji na kuchochea shughuli za uchenjuaji madini. Pia, amezungumzia upanuzi wa gridi ya taifa unaotekelezwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) katika maeneo ya madini, kwa lengo law kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika kwa wawekezaji na wachimbaji.
Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Chemba ya Migodi Tanzania Mhandisi Benjamin Mchampaka akizungumzak atika mahojiano maalum amesema kikao hicho kimekuwa ni muhimu kwa kuwa pamoja na mambo mengine, kimetoa fursa kwa mawaziri kujadili kwa pamoja changamoto zinazozuia uwekezaji zaidi Afrika ikilinganishwa na utajiri ambao bara hilo limejaliwa.
‘’ Suala la kuongeza thamani madini hususan madini muhimu na mkakati limepewa mkusumo mkubwa kwamba ni wakati sasa wa kuwa na mikakati ya pamoja kama Sera za pamoja kuhakikisha tunaongeza thamani madini kwenye nchi zetu ili Madini haya yawe na manufaa zaidi kwa wananchi na Taifa huku huku Sekta zote tukishirikiana, Serikali na binafsi," amesema Mchwampaka.
Kikao hicho cha Mawaziri katika kongamano la Mining Indaba kimejikita katika kujadili mikakati mbalimbali ya ushirikiano kati ya Serikali na Sekta Binafsi, huku suala la madini mkakati likichukua nafasi kubwa ya majadiliano kama nyenzo muhimu ya maendeleo ya kiuchumi barani Afrika.
#Uongezajithamanimadini
#ValueAddition
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.