[Latest Updates]: Wizara ya Madini Kuanza Utoaji wa Huduma Ndani ya Jengo Piya Kuanzia Mwei 15, 2025

Tarehe : March 20, 2025, 1:57 a.m.
left

• Kamati ya Bunge Yasema ina matumaini Makubwa na Hatua iliyofikiwa, Wapongeza Serikali kutoa fedha

• Ujenzi Wafikia Asilimia 92.8

Dodoma

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde ameiambia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na  Madini kwamba, ifikapo Mei 15, 2025, Huduma zote za Wizara Makao Makuu, zitaanza kutolewa katika Jengo Jipya la Wizara Mji wa Serikali- Mtumba baada ya michakato yote kukamilishwa.

Amesema hayo leo Machi 20, 2025, wakati wa ziara ya Kamati hiyo ilipotembelea kukagua maendeleo ya mradi huo ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 92.8, huku kazi chache zilizobaki zikihusisha ukamilishaji wa masuala ya mifumo ya TEHAMA, zimamoto, rangi na samani za ndani ambapo tayari Wizara imekwisha kutangaza zabuni ya samani hizo.

‘’Mhe. Mwenyekiti, kukamilika kwa jengo hili kutaiwezesha Wizara kuwahudumia watanzania na wageni kutokea eneo moja na hivyo  kutoa huduma kwa urahisi kuliko ilivyo sasa ambapo baadhi ya watumishi wako kwenye maeneo mengine ikiwemo katika eneo la ilipo Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na hapa Mtumba,’’ amesema Mhe. Mavunde.

Ametumia fursa hiyo kuishukuru Serikali kwa kwa kuweka nguvu ili kukamilisha mradi wa Mji wa Serikali na kuweza kutoa kiasi cha shilingi bilioni 300 kwa ajili ya ujenzi wa mji huo na kueleza kuwa, uwepo wa mji huo utasaidia kurahisisha utoaji huduma kwa Serikali na kuongeza kwamba, umeongeza mwonekano  mzuri  wa mji  wa Dodoma huku akitolea mfano wa Nchi ya Malaysia kuwa na mfumo kama Mtumba.

Naye, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Dkt. David Mathayo amesema kwamba Kamati hiyo ina matumiani makubwa kutokana na hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa jengo hilo na hivyo kutoa pongezi kwa Serikali kwa kutoa fedha kukamilisha majengo yaliyopo katika mji huo na kusema kwamba  uwepo wa Wizara zote katika mji huo utarahisisha utoaji huduma kwa wawekezaji na watanzania  kama ilivyo kwa nchi ya Brazil.

Katika hatua nyingine, Mhe. Dkt. Mathayo ameumwagia sifa uongozi wa Wizara ya Madini kutokana na namna wanavyosimamia shughuli za Sekta ya Madini na kueleza kuwa, kitendo hicho kinatoa ahueni kwa kamati hiyo ambayo inasimamia Wizara za Madini na Nishati.

‘’Tunawafahamu namna mnavyochapa kazi, kamati yetu tuna furahi tuna viongozi walionyooka, ni viongozi, wazoefu na wachapakazi. Hatuna shaka kama kamati tunafurahi kwasaabu mnaisimamia wizara vizuri,’’ amesema Dkt. Mathayo.

Awali, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu Wizara ya Madini, Festus Mbwilo akisoma taarifa ya maendeleo ya mradi, ameieleza kamati kuwa Wizara imeendelea kusimamia kwa karibuni utekelezaji wa mradi huo ulioanzamwaka 2021 ili ukamilike kwa wakati ikiwemo kuchukua hatua za kukabiliana na changamoto zinazojitokeza

Mkandarasi wa jengo la Wizara ya Madini ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na linajengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 22.8 na Mshauri Elekezi ni Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals