[Latest Updates]: Zaidiya Watu 58 wanufaika na Programu ya usimamizi wa Maji taka Migodini

Tarehe : Oct. 9, 2025, 3:43 p.m.
left

Zaidi ya watu 58 wamenufaika na programu ya usimamizi wa maji taka migodini, inayotekelezwa kuanzia mwaka 2018 hadi 2025 chini ya usimamizi wa Taasisi ya Jiolojia ya Sweden (SGU) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (SIDA).

Hayo yamesemwa leo Oktoba 2, 2025 na Meneja wa Mradi wa Mafunzo ya Kimataifa kutoka SGU, Bi. Jonnina Karlsson, wakati wa ziara yake katika Ofisi za Wizara ya Madini na kushiriki kikao kilichoongozwa na Kamishna wa Madini, Dkt. AbdulRahman Mwanga, jijini Dodoma.

Katika kikao hicho, Bi. Karlsson ameeleza kuwa hivi karibuni kutakuwa na fursa nyingine kupitia mradi wa PanGeo+ ambao utatoa mafunzo kwa wataalamu wa Sekta ya Madini, hususan katika masuala ya kiufundi na usimamizi endelevu wa mazingira.

Aidha, Bi. Karlsson ameonesha nia ya kufahamu mahitaji ya wataalamu wa Sekta ya Madini nchini, ambapo imebainishwa kuwa miongoni mwa mahitaji hayo ni pamoja na mwongozo wa ufungaji wa migodi kwa wachimbaji wadogo; Upimaji wa maji taka kabla ya kurejeshwa kwenye mazingira, hasa kwa wachimbaji wadogo na Matumizi ya teknolojia za Remote Sensing na mifumo ya taarifa za jiolojia (GIS) katika utafutaji wa madini pamoja na kujenga uwezo wa watalaam katika mchakato wa kisayansi na kiuhandisi hususan katika kutathmin.

Mahitaji mengine ni kujengewa uwezo katika kupanga na kuonyesha kiasi cha ubora wa rasilimani kama vile madini yaani  Resource modelling kwa ajili ya kusaidia kufanya maamuzi sahihi katika utekelezaji wa miradi ya madini.

Kwa upande wake, Kamishna wa Madini Dkt. Abdulrhaman Mwanga ameishukuru SIDA kupitia SGU kwa kuwezesha mafunzo hayo ambayo yamelenga kuongeza uelewa kwa wataalamu wa madini kuhusu usimamizi wa madini pamoja na miundombinu ya maji taka migodini, hatua inayosaidia kulinda mazingira na kukuza uchimbaji endelevu.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals