[Latest Updates]: Kwanini Wizara ya Madini Kila Mwaka Inaboresha Ushiriki Wake Katika Maonesho ya Kimataifa ya Kibiashara?

Tarehe : July 7, 2025, 12:34 p.m.
left

7/7/2025

Dar es salaam

Ikiwa mwaka wa 49 wa maonesho ya kibiashara ya kimataifa maarufu kama Sabasaba ambapo Wizara ya Madini na Taasisi zake imekuwa ikishiriki kwa kipindi chote huku ikiendelea kuongeza ubunifu  na kuboresha ushiriki wake katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es salaam.

Kwa mwaka huu wa 2025 maonesho yanabebwa na kaulimbiu inayosema.

" Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba,fahari ya Watanzania" 

Lengo kubwa la Wizara ya Madini na taasisi zake kuongeza ubunifu katika maonesho hayo ni kuwajumuisha Watanzania katika mnyororo wa thamani madini pamoja na ;

Kuongeza utambulisho na kunadi fursa za uwekezaji kimataifa kupitia jukwaa 
kubwa la kimataifa linaloendeshwa na TanTrade, likiihusisha sekta mbali mbali ikiwemo madini, kilimo , maji na nishati .

Kupitia jukwaa la kibiashara la  Sabasaba  wawekezaji wa ndani na kimataifa kutoka kona mbalimbali za dunia huvutiwa kufika katika banda la wizara na taasisi ili kupata  uelewa wa mambo mbalimbali kupitia machapisho yenye taarifa zinazoelezea mnyororo mzima wa thamani madini kuanzia ngazi ya utafiti ,  uchimbaji , uchakataji hadi usafirishaji.

Kwa mwaka huu wa 2025, Wizara imewekeza katika ujumuishaji wake katika maonyesho pamoja na taasisi zake (STAMICO, Tume ya Madini, GST, TEITI), ili kuonyesha jinsi mnyororo wa thamani unavyofanya kazi pamoja na fursa nyingine zinazoambatana na Sekta ya Madini.

Kupitia ushiriki huu, pia Wizara kwa kushirikiana na taasisi zake inaonyesha hatua zake za mnyororo wa thaman madini  kwenye uchimbaji,  uchakataji na  uendelezaji  madini  kabla ya kusafirishwa nje ya nchi.

Kama inavyofahamika kuwa, Wizara imewekeza kwenye minada ya madini ya vito, ikiwa ni pamoja na kuanzisha mfumo wa kielektroniki pamoja na minada katika maeneo maalum kama Mirerani ili kuongeza uwazi na ushindani wa bei.

Kuongeza kiwango cha uwazi kinachoenda sambamba na elimu inayotolewa wakati wa maonyesho kuhusu udhibiti wa rasilimali madini, Utoaji wa leseni, ukaguzi na usalama wa migodi.

Kuonyesha utekelezaji wa mikakati ya uwazi, uchumi wa thamani madini na  minada ya madini kupitia mifumo ya  kielektroniki,

Kuimarisha Mpango wa Serikali wa Ukusanyaji maduhuli na ongezeko la thamani madini.

Kuongeza uelewa kwa wadau kuhusu fursa, sheria, na teknolojia zinazohusiana na mnyororo wa thamani madini.

Kuwaeleza wadau jinsi Wizara ya Madini na taasisi zake  inavyoongeza  uwezekaji wa kipato na  mchango wa Sekta ya Madini katika maendeleo ya kiuchumi, ajira kwa  watanzania, na kukuza ushirikishwaji wa wadau wote nchini.

#GDP: 10.1 FromMineralSector
#MineralValueAddition
#InvestInMiningSectorTz

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals