Tarehe : July 4, 2025, 12:13 p.m.
Wizara ya Madini, kwa kushirikiana na taasisi zake inaendelea kutoa elimu ya kina kuhusu shughuli za madini katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Katika banda la Wizara hiyo, wananchi, wawekezaji na wanafunzi wanapata fursa ya kipekee kujifunza kuhusu sekta ya madini nchini, kuanzia uchimbaji, uchenjuaji, usimamizi wa mazingira, hadi masuala ya usafirishaji na masoko ya madini.
Akizungumza katika maonesho hayo, Mjolojia kutoka Wizara ya Madini Neema Masinde amesema lengola uwepo wa Wizara ya Madini na Taasisi zake ni kuhakikisha wananchi wanaelewa mchango wa sekta ya madini katika uchumi wa nchi, lakini pia kuwapa maarifa sahihi juu ya fursa zilizopo ili waweze kushiriki kikamilifu.katika shughuli za madini.
Masinde ameongeza kuwa, elimu inayotolewa katika maonesho hayo inalenga kuwahamasisha wananchi kushiriki kwa tija katika sekta hiyo, kwa kuwa ni mojawapo ya sekta zinazochangia kwa kiasi kikubwa katika pato la taifa (GDP) na ajira.
Maonesho ya Sabasaba mwaka huu yamevutia washiriki kutoka zaidi ya nchi 40, huku banda la Wizara ya Madini likiwa ni miongoni mwa mabanda yaliyovutia idadi kubwa ya wageni kutokana na mvuto wa sampuli za madini na elimu inayotolewa moja kwa moja na wataalam.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.