[Latest Updates]: Kasi ya Ujenzi wa Viwanda vya Kuongeza Thamani Madini Yaongezeka Nchini Tanzania

Tarehe : Aug. 26, 2025, 3:16 p.m.
left

Waziri Mavunde aweka Jiwe la Msingi Kiwanda cha Kusindika na Kuyeyusha Nikeli na Shaba - Dodoma

Ni maelekezo ya Mhe. Rais Samia kuyaongezea thamani madini ndani ya nchi.

Mradi kuchakata takribani tani  200,000 za nikeli na Shaba kwa mwaka

Dodoma, Tanzania 

Serikali imeendelea kuthibitisha dhamira yake ya kuhakikisha rasilimali za madini zinawanufaisha Watanzania kupitia uongezaji thamani ndani ya nchi ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha uchumi wa kijani (green economy)  hususan katika utengenezaji wa magari ya umeme, betri za magari, nishati safi na vifaa vya kielektroniki.

Hayo yamewekwa wazi leo Agosti 26, 2025 na Waziri wa Madini, Mhe. Anthony  Mavunde, wakati akiweka jiwe la msingi la Kiwanda cha kusafisha na kusindika Madini ya Nikeli na Shaba kinachojengwa na Kampuni ya Zhongzhou Mining Co. Ltd, eneo la Zamahero, Wilaya ya Bahi, mkoani Dodoma.

Amesema kuwa, Mradi huo utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwamba madini yanayochimbwa hapa nchini yaongezewe thamani ndani ya nchi na kuuza bidhaa ya mwishyabadala ya madini ghafi.

“Ujenzi wa kiwanda hiki ni uthibitisho kuwa dhamira ya kuongeza thamani madini nchini, tunataka kuona Tanzania ikibadilika na kuwa taifa linalozalisha bidhaa zenye thamani kubwa kwenye soko la dunia la bidhaa teknolojia.” amesema Mavunde 

Waziri Mavunde ameeleza kuwa mradi huo wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 15 utakapokamilika utazalisha takribani tani 200,000 za nikeli na shaba kwa mwaka, kuajiri zaidi ya Watanzania 200 hadi 230, na kuchangia kodi na mapato mengine ya Serikali.

“Uwekezaji huu ni kielelezo cha mafanikio ya Serikali katika kufanikisha dira ya uchumi wa viwanda na uongezaji thamani madini kama ilivyoelekezwa na Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020–2025," amesisitiza Mavunde. 

Amebainisha kuwa, pia Sera ya Madini ya mwaka 2009 inaelekeza kuyaongezea thamani madini yetu ndani ya nchi na kuongeza kuwa “hivi sasa Tanzania tuna viwanda vinane vya kusafisha madini ya dhahabu (gold refinery) lakini viwanda vya kuongezea thamani Madini ya metali tunavyo 9, mkoa wa Dodoma peke yake tunavyo vitano”  ameongeza Mavunde. 

Kwa upande wake, Kamishna wa Madini, Dkt. AbdulRahman Mwanga amesema kuwa, kwa kuwekeza kwenye miradi ya kuongeza thamani, Tanzania inajenga msingi imara wa ajira, mapato, na uchumi shindani kimataifa na kufikia lengo la ujenzi wa Tanzania ya uchumi.

Naye, Mkurugenzi wa Kampuni ya Zhongzhou Mining Lee Zhong LIANG amemuhakikishia Waziri Mavunde kuwa Kampuni itaendeleza uhusiano mwema na Serikali pamoja wananchi wanaozunguka mradi huo.

Pia, Katibu Tawala Wilaya ya Bahi , Mwanamvua Muyongo ameeleza kuwa uwepo wa kiwanda hicho utasaidia kuiweka Wilaya hiyo katika ramani ya wazalishaji wa bidhaa muhimu za kiteknolojia pamoja na kuboresha maisha ya watu wa hapa kupitia ajira rasmi na zisizo za moja kwa moja.

*#Value Addition
For Socio- Economic Development*

#Uongezaji Thamani Madini kwa  Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals