Tarehe : March 17, 2022, 1:05 p.m.
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko amekutana na Rais wa Baraza la Uchumi na Jamii la Umoja wa Mataifa (ECOSOC), Bw. Collen Kelapile katika kikao kilicholenga kupata maelezo kabla ya kushiriki kikao cha Baraza la Uchumi na Jamii la Umoja wa Mataifa kitakachofanyika tarehe 18 Machi, 2022, katika Ukumbi wa Umoja wa Mataifa, jijini New York, Marekani.
Tanzania inashiriki katika kikao hicho ikiwa ni Mwenyekiti wa Nchi Wazalishaji wa Madini ya Almasi Afrika ( ADPA).
Aidha, kikao hicho kinalenga kujadili namna bora za kutumia rasilimali katika nchi husika kuibua maendeleo jumuishi kwenye jamii ambazo maliasili hizo zinapatikana ili zisaidie kuleta amani na hatimaye kufikiwa maendeleo endelevu.
Kikao hicho kitafanyika chini ya mada isemayo "Maliasili Jamii yenye Amani na Maendeleo Endelevu: *Mafunzo kutoka kwenye Mchakato wa Kimberley
Wengine wanaoshiriki kikao hicho katika picha ni pamoja na Waziri wa Madini wa Zimbabwe Wiston Chitando ambaye ni Makam Mwenyekiti wa ADPA, Mratibu wa Kimberly Afrika Bw. Jacob Thamage na Mwakilishi wa Kudumu Umoja wa Mataifa, Balozi Prof. Kennedy Gastorn.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.