[Latest Updates]: Wataalamu Sekta ya Madini Kukutana na Wataalamu wa DRC

Tarehe : June 23, 2022, 5:23 p.m.
left

Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko amesema Wizara anayoiongoza iko tayari kutoa wataalamu wake ili wakakutane na wataalamu wa Jamhuri ya

Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa lengo la kujadili namna bora ya kushirikiana katika biashara na mnyororo mzima wa biashara ya madini.

Dkt. Biteko ameyasema hayo kwenye kikao chake na Gavana wa Katanga kutoka DRC Jacques Katwe pamoja na ujumbe wake jijini Dodoma.

Aidha, Dkt. Biteko amesema, kutokana na utajiri wa madini uliopo nchini Tanzania, Mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa umeendelea kuimarika kutoka asilimia 4.7 mwaka 2019 hadi kufikia asilimia 7.9 Septemba mwaka 2021.

Dkt. Biteko amesema Sekta ya Madini kwa miaka mitatu mfurulizo imekuwa ikiongoza katika kuliingizia Taifa fedha za kigeni.

“Tumeondoa urasimu kwenye biashara ya madini, mfanyabiashara akiomba kibali cha kusafirisha madini atapewa kibali kwa wakati, hivyo nitumie fursa hii kukuomba Mhe. Gavana kuwaleta wawekezaji kuja kuwekeza kwenye Sekta ya Madini,” amesema Dkt. Biteko.

Aidha, Dkt. Biteko amesema ujenzi wa kiwanda cha kusafisha madini ya dhahabu cha Mwanza Precious Metal Refinery kitawasaidia wafanyabishara wa madini wa DRC kusafisha madini yao ambapo ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wafanyabiashara wa madini wa DRC kuja Tanzania kusafisha madini yao.

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Biteko amesema Tanzania inautajiri mkubwa wa madini ambapo wizara inajitahidi kusimamia Sheria, Kanuni na Taratibu ili madini hayo yaweze kuwanufaisha wananchi kwa kubadilisha maisha yao kiuchumi na kuwapatia ajira.

Kwa upande wake, Gavana wa Katanga wa DRC Jacques Katwe amempongeza Waziri wa Madini kwa usimamizi madhubuti anaoufanya katika kuiongoza wizara hiyo ambayo imepata mafanikio makubwa.

“Lengo la ziara hii ni kujifunza jinsi gani Tanzania imefanikiwa kwenye Sekta ya Kilimo hivyo tukaona bora tufike na Wizara ya Madini ili tujifunze baada ya kutambua utajiri wa madini tulionao DRC na utajiri wa madini yaliyopo Tanzania,” Katwe amesema.

Sambamba na hayo, Katwe amefurahishwa na ujenzi wa kiwanda cha kusafisha madini ya dhahabu cha Mwanza Precious Metal Refinery ambapo amesema atahakikisha anawasisitiza wafanyabiashara wa madini kuleta madini yao Tanzania kwa ajili ya kusafishwa.

Naye, Kamishna wa Madini Dkt. Abdulrahaman Mwanga amepata fursa ya kumueleza Gavana Katwe na ujumbe wake aina za madini zilizopo nchini Tanzania na kuwaeleza jinsi gani shughuli za uchimbaji, uchenjuaji, na uongezaji thamani madini zinavyofanyika ikiwemo Ujenzi wa Kiwanda cha kusafisha madini ya dhahabu cha Mwanza Precious Metal Refinery.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals