[Latest Updates]: Ghana Yavutiwa na Mpango wa Uwazi, Uwajibikaji Sekta ya Madini Tanzania

Tarehe : Dec. 4, 2023, 8:29 a.m.
left

# Wafurahishwa na mchango wa wachimbaji wadogo

# Waipongeza TEITI kwa kutoa ripot 13 za Uwazi na Uwajibikaji

Ujumbe kutoka Taasisi ya Uhamasishaji, Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini na Gesi Asilia nchini Ghana (GHEITI) umefurahishwa na utekelezaji wa mpango wa Uhamasishaji, Uwazi na Uwajibikaji jinsi unavyotekelezwa nchini Tanzania katika mnyororo wa maendeleo ya sekta ya Madini.

Hayo yamesemwa leo Disemba 4, 2023 na Mwenyekiti Mwenza wa GHEIT Dkt. Steve Manteaw mapema baada ya kupokea taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa Taasisi ya  Uhamasishaji, Uwazi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Uziduaji Rasilimali Madini ,
Gesi Asilia na Mafuta (TEITI)  katika mkutano wa kubadilishana uzoefu wa kikazi uliofanyika jijini Dodoma.

Akizungumza katika mkutano huo Dkt. Manteaw amesema kuwa Tanzania kupitia taasisi ya TEITI imekuwa mfano bora kwa  kusimamia shughuli za TEITI kwa kutekeleza vigezo vya Kimataifa kama mpango wa Jumuiya ya Kimataifa ya Uwazi, Uwajibikaji na Uhamasishaji (EITI) unavyoelekeza kwa nchi wanachama.

Dkt. Manteaw amefafanua kuwa jumuiya ya EITI inawachama zaidi ya 57 lakini wamevutiwa na Tanzania ambapo inaonekana kuwa nchi ya mfano mzuri katika uwasilishaji wa ripoti zake ukilinganisha na nchi nyingine ambazo ni wanachama.

Kuhusu mchango wa wachimbaji wa madini nchini , ujumbe huo umevutiwa na mchango wa wachimbaji wadogo kwa kufikia asilimia 40 ya mchango wao ndani ya Sekta hii, huku wakiahidi kuwa wakifika nchini Ghana wataishauri Serikali kuiga mipango shirikishi inayotumika Tanzania ili itekelezwa nchini humo. 

Kwa upande wake mwenyekiti wa TEITI  Bw. Ludovick Utouh amesisitiza kuwa pamoja mabadiliko ya kupiga hatua katika Uwajibikaji, Uwazi na Uhamasisha katika usimamizi Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia itaendelea kutengeneza mifumo yake ya ripoti ya kimtandao ili wadau wa sekta husika ndani na nje nchi wapate taarifa za malipo ya kampuni pamoja na mapato ya Serikali kutoka katika kampuni husika.

Utouh ameongeza kuwa kwa kuzingatia kanuni za kimataifa kupitia EITI kwenye sekta ya Uziduaji itazingatia uwazi katika masuala ya mazingira ili kuongeza usimamizi na uwajibikaji wa kimazingira ndani ya sekta hiyo.

Katika mkutano huo Tanzania imewakilishwa na wataalam kutoka taasisi zilizo chini ya Wizara ya Madini ikiwemo Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Tume ya Madini, Ofisi ya Kamishna wa Madini, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Ujumbe wa watu kumi na mmoja kutoka taasisi ya GHEITI  upo nchini Tanzania kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali ndani ya Sekta ya Madini .

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals