[Latest Updates]: Timu ya Kamba Madini Yaibuka Kidedea Kuelekea Mei Mosi Singida

Tarehe : April 17, 2025, 7:16 p.m.
left

Timu ya michezo ya Wizara ya Madini imeendelea kung'ara katika mashindano ya michezo ya Mei Mosi kwa mwaka 2025, yanayoendelea kufanyika mkoani Singida. Michezo hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani na hushirikisha taasisi mbalimbali za umma.

Katika michezo hiyo ya makundi iliyoanza rasmi tarehe 16 Aprili 2025, Timu ya Kamba Wanawake ya Madini leo Aprili 17, 2025 imeonyesha uwezo wa hali ya juu kwa kuibuka na ushindi dhidi ya Timu ya Utamaduni, baada ya kuvuta mivuto miwili mfululizo na kujikusanyia alama mbili muhimu.

Aidha, Timu ya Kamba Wanaume ya Madini Sports Club nayo haikuachwa nyuma, ambapo katika mechi kali dhidi ya UCSAF, walifanikiwa kupata ushindi wa mivuto miwili kwa sifuri na hivyo kujizolea pointi mbili.

Katika mchezo mwingine wa awali uliofanyika Aprili 16, 2025, Timu ya Kamba Wanawake ya Madini Sports Club ilikabiliana na Afya Sports Club, ambao ni washindi wa pili wa mashindano ya Mei Mosi ya mwaka 2024 ambapo katika mchezo huo wa kusisimua, mvuto wa kwanza uliibeba Madini, huku mvuto wa pili ukienda kwa Afya, na hivyo timu zote mbili kugawana alama 1 – 1.

Mbali na michezo ya kuvuta kamba, mashindano hayo pia yanajumuisha michezo mingine ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa pete (netiboli), mpira wa wavu (volleyball), mpira wa kikapu (basketball), riadha, bao, drafti na karata.

Mashindano haya hufanyika kila mwaka kama sehemu ya kuimarisha mshikamano miongoni mwa wafanyakazi, kukuza afya kupitia michezo, na kusherehekea mafanikio ya kazi na uzalendo kuelekea kilele cha maadhimisho ya Mei Mosi.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals