[Latest Updates]: Bilioni 18 zimetumika miradi ya “CSR” Mkoani Geita

Tarehe : Nov. 19, 2019, 7:56 a.m.
left

Na Issa Mtuwa – “WM” Geita

Waziri wa Madini  Doto Biteko amesema anaridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya  jamii (Corporate Social Responsibility - CSR) inayotekelezwa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita – GGM ikiwa na madhumuni ya kuifanya jamii inayo zunguka mgodi huo kufaidika kutokana na uwepo wa raslimali hiyo.

“Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Yapo mambo bado sikubaliani nao hasa kwenye masuala ya Local Content hususani ajira, mishahara ya watanzania na huduma na manunuzi bado sijaridhishwa. Lakini kuhusu CSR niseme ukweli GGM wanafanya vizuri sana”. Alisema Biteko wakati akiweka jiwe la msingi la jengo la Zahanati ya Magereza Geita miongoni mwa miradi ya CSR Geita mjini.

Biteko alisema GGM wamejenga, zahanati kadhaa ikiwemo hiyo ya Magereza Geita, vyumba vya madarasa, barabara za lami, taa za barabarani, ujenzi wa soko kubwa la wamachinga geita, soko kuu la dhahabu na mirandi mingine, vyote hivyo ni miradi ya CSR inayotekelezwa na fedha za GGM.

“Hii ndio namna ya kuweka alama hata kwa vizazi vijayo kuyafanya madini kuishi na hata madini na mgodi wa GGMM kufungwa. GGM wameshatumia fedha nyingi za CSR zaid ya bilioni 18 kwa ajili ya miradi katika maeneo yetu ya Geita. Fedha hizi nyingi sana huko nyuma kabla ya serikali ya awamu ya tano hazijawahi kutolewa na huko nyuma mgodi ulikuwa unapanga nini cha kufanya lakini leo miradi hii inayotekelezwa inatokana na mipango na vipau mbele vya Halmashauri zenyewe na kumbwa utekelezaji wake unashiriki serikali zetu za mitaa”. Alisema Biteko.

Ameongeza kuwa, zoezi la uwekaji wa jiwe la msingi la Zahanati hiyo ya Magereza tarehe 18/11/2019 ni moja ya kielelezo hicho na amefurahi kusikia ujenzi huo unaendelea na utakamilika bila kukwama. .

“Naomba nitumie fursa hii, kuwakumbusha wenye leseni za uchimbaji madini kote nchini watambue CSR ipo kwa mujibu wa sheria na kila mwenye leseni popote alipo ana wajibu wa kuchangia maendeleo ya jamii kwenye eneo la leseni ilipo, sio suala la migodi mikubwa pekee,” aliongeza Biteko.

Akisoma taarifa ya ujenzi wa Zahanati hiyo, mkuu wa Gereza Geita, SSP. Mussa Mkisi alimwambia mgeni rasmi Waziri wa Madini Doto Biteko kuwa ujenzi huo unaendelea vizuri  na jumla Tshs. milioni 50,000,000/- zimetengwa kutoka mfuko wa CSR –Geita mjini kukamilisha ujenzi huo. Aliongeza kuwa hadi kukamilika kwake, ujenzi huo utakamilika kwa  gharama ya jumla ya Tshs. milioni 170,000,000/- na Zahanati hiyo ya kisasa itakuwa inatumiwa na wafungwa, mahabusu na jamii nzima inayozunguka Zahanati hiyo.

Kwa upande wa mgodi wa GGM kupitia Mkurugenzi Mtendaji  wa mgodi, Richard Jordanson amesema wanaona fahari kutekeleza miradi inayo walenga wananchi wote moja kwa moja kwani miradi hiyo inakuwa ni kielelezo na kwamba wataendelea kutekeza miradi mbalimbali kwa kuzingatia miongozo ya utekelezaji wake.

Jordanson ameongeza kuwa mgodi wa GGM utaendelea kushirikiana na serikali huku akimuahidi Waziri wa Madini kumshangaza kwa maajabu atakayoyafanya kuhusu utekelezaji wa Local content katika mwaka ujao.

Wakati huo huo Waziri wa Madini Doto Biteko ametoa kiasi cha Tsh. Milioni 1,500,000/- kwa ajili ununuzi wa mchele, Ng’ombe na Vinywaji baridi kwa ajili ya wafungwa na mahabusu wa gereza hilo kwa siku hiyo. Ametoa fedha hiyo alipotembea Gerezani hapo na kuzungumza nao, huku akiwatia moyo kwamba wasivunjike moyo na kwamba mungu anampenda kila mtu na siku moja watarudi uraiani.

Nae Mbunge wa Geita mjini na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu amewafariji kwa kuwaambia wasikate tama na kwamba hata walioko nje ni wafungwa au mahabusu watarajiwa huku akibainisha kuwa hata yeye aliwahi kukaa mahabusu siku tano baada ya yeye na wenzake kufanya fujo na vurugu wakiwa shuleni lakini leo maisha yanaendelea.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals