Tarehe : May 8, 2018, 10:17 a.m.
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki amezindua mkutano wa baraza la kwanza la wafanyakazi wa Wizara ya Madini mjini Morogoro wenye lengo la kujadili utendaji kazi na namna ya kukabiliana na changamoto katika sekta ya madini.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Madini wakiimba wimbo maarufu wa mshikamano (solidarity forever) kwenye mkutano huo
Katika mkutano huo Waziri Kairuki amewataka watumishi kuelekeza nguvu kwenye kutoa kipaumbele kwenye masuala muhimu kama vile kuendelea kutengeneza sera bora zinazosimamia rasilimali za madini na kuweka mfumo mzuri na ulio bora wa ukusanyaji wa mapato ili sekta ya madini iwe na mchango mkubwa katika Pato la Taifa.
Pia, amewapongeza watumishi kwa ukusanyaji wa maduhuli hadi kuvuka lengo kwa asilimia 130 ya makusanyo ya lengo lililokuwa limewekwa kwenye Sekta ya Madini.
Aidha, amewataka watumishi kurekebisha kasoro zilizojitokeza katika utekelezaji wa bajeti ya Mwaka 2017/2018 ili kufanya vizuri kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019
Aidha amewaasa watumishi wote kuwa waadilifu katika utendaji kazi wa kila siku na kuagiza watumishi wote waelimishwe kuhusu maadili katika utumishi wa umma na wale ambao hawajajaza fomu za maadili kujaza mara moja.
Naye Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko amesema Wizara imebeba matarajio makubwa ya wananchi na kuwataka watumishi kufanya kazi kwa weledi ili kuleta matokeo chanya.
Aidha, amesema Wizara ya Madini ni miongoni mwa Wizara zinazowajibika kuchangia kwa kiwango kikubwa katika Pato la Taifa.
Sekretarieti ya maandalizi katika mkutano huo.
Waziri Biteko amesisitiza mahusiano mazuri baina ya vyama vya wafanyakazi na waajiri ili Sekta ya Madini iwe na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi.
Masuala yaliyojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na umuhimu wa baraza la wafanyakazi, muundo wa Wizara ya Madini na maadili katika utumishi wa umma. Masuala mengine yaliyojadiliwa ni pamoja na mapitio na utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018, mpango wa bajeti wa mwaka 2018/2019 na marekebisho ya Sheria ya Madini ya mwaka 2017.
Mkutano huo umefanyika leo tarehe 07 Mei, 2018 katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) mjini Morogoro.
Imeandaliwa na:
Greyson Mwase,
Afisa Habari,
Wizara ya Madini,
5 Barabara ya Samora Machel,
S.L.P 2000,
11474 Dar es Salaam,
Simu: +255-22-2121606/7, Nukushi: +255-22-2121606,
Barua Pepe: info@madini.go.tz,
Tovuti: madini.go.tz
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.