[Latest Updates]: Dkt. Kiruswa Atoa Rai kwa Menejimenti Wizara ya Madini Kutatua Changamoto za Wafanyakazi

Tarehe : April 9, 2024, 10:22 p.m.
left

Naibu Waziri wa Madini, Dkt Steven Kiruswa ametoa rai kwa Menejimenti ya Wizara ya Madini kuhakikisha inachukua hatua za dhati katika kutatua changamoto ambazo zinawakabili Watumishi wa Wizara na kuzifanyia kazi ili kuongeza ufanisi katika kutekeleza majukumu yao.

Alitoa rai hiyo Aprili 8, 2024, wakati akifunga Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Madini lililofanyika Mji wa Serikali Mtumba – Jijini Dodoma 

Dkt. Kiruswa alisema kuwa, ni muhimu Menejimenti kukumbuka mara zote kuwa watumishi ndiyo hazina kuu ya kutekeleza, kusimamia na kuhakikisha malengo yaliyowekwa ya Wizara na Sekta ya Madini yanatimia. 

“Ni vyema tukaijali hazina hiyo. Aidha, ni vema kwa Menejimenti ya Wizara kuchukua hatua katika kutatua changamoto ambazo zinalalamikiwa na Watumishi wa Wizara na kuzifanyia kazi. Ni matumaini yangu kuwa mtazingatia yale mliyoyapata katika Mkutano huu na nisisitize suala la uwajibikaji na uzingatiaji wa sheria na kanuni katika utekelezaji wa majukumu yetu” amesema Dkt. Kiruswa.

Pia Naibu Waziri Dkt. Kiruswa alisistiza kuhusu kutekeleza maelekezo aliyoyatoa Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo ili kuwezesha Maendeleo ya Sekta. Awali, Waziri Mavunde alisisitiza kuongeza ubunifu na kwamba milango yake iko wazi kwa Watumishi kumshauri kwa manufaa ya Wizara na Sekta ya Madini.

Kwa upande wake, Mweyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Madini na Naibu Katibu Mkuu Msafiri Mbibo alisema kuwa Wizara itaendelea kuboresha mazingira ya kazi kwa Watumishi huku akiahidi kuwa Menejimenti itafanyia kazi maelekezo ya Waziri kuhusu kusikiliza na kutatua changamoto za Wafanyakazi sambamba na kuendelea kuwajengea uwezo ili kuongeza ufanisi katika kutekeleza majukumu yao.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals