[Latest Updates]: Madini Yagusa Makundi Nje ya Mnyororo wa Thamani Madini

Tarehe : Aug. 7, 2025, 11:10 a.m.
left

Dkt. Serera atoa wito kwa GST kufanya Tafiti

STAMICO kuzalisha na kusambaza Rafiki Briquettes nchi nzima

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera, ameipongeza Wizara ya Madini kwa juhudi zake za makusudi katika kupanua wigo wa wanufaika wa rasilimali za madini nchini, kwa kuanzisha na kutekeleza mikakati inayogusa makundi ambayo hapo awali hayakuwa sehemu ya moja kwa moja ya mnyororo wa thamani wa madini.

Akizungumza katika banda la Wizara ya Madini na Taasisi zake kwenye maonesho ya Nanenane yanayoendelea  jijini Dodoma, Dkt. Serera amesema kuwa hatua hiyo ya Wizara ya Madini si tu kwamba inaongeza ushiriki wa wananchi katika uchumi wa madini, bali pia inatoa fursa kwa watanzania wengi zaidi kunufaika na utajiri wa rasilimali hizo kwa njia mbalimbali.

“Napenda kutoa pongezi za dhati kwa Wizara ya Madini na Taasisi zake kwa kuendelea kuonesha dira ya wazi ya kuhakikisha kuwa rasilimali za madini hazinufaishi tu wachimbaji au wawekezaji wa moja kwa moja, bali pia makundi mengine kama wanawake, vijana, wajasiriamali wadogo, wasanii wa uchoraji na ufinyanzi, na hata sekta ya huduma kama usafirishaji, malazi, na chakula,” amesema Dkt. Serera.

Amesisitiza kuwa ushirikiano kati ya sekta ya madini na sekta ya viwanda na biashara ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya viwanda vya ndani vinavyotegemea malighafi kutoka kwenye sekta hiyo, hivyo mkakati wa kuiunganisha jamii kwa upana zaidi unapaswa kuungwa mkono na kuendelezwa kwa nguvu zaidi.

Kwa upande mwingine, ametoa wito kwa sekta binafsi, mashirika ya kijamii na taasisi za elimu kushirikiana na Serikali katika kuibua na kukuza fursa zilizopo kwenye maeneo ya usindikaji, ubunifu wa bidhaa za madini, pamoja na biashara ya bidhaa zinazotokana na madini kwa kutumia teknolojia na mbinu bunifu za kisasa.

Wizara ya Madini imekuwa ikitekeleza Sera na mikakati mbalimbali ikiwemo utoaji wa mafunzo, kusaidia kupata mikopo kwa wachimbaji wadogo, kuendeleza masoko ya madini, pamoja na kuwaunganisha wadau wa sekta ya madini na masoko ya ndani na ya kimataifa. Mikakati hii imeleta mafanikio makubwa katika kuleta uwiano wa manufaa ya rasilimali za taifa kwa wananchi kwa ujumla.

Hatua hiyo ya kuwajumuisha watu nje ya mnyororo wa kawaida wa uzalishaji wa madini imeelezwa kuwa ni ya kimkakati na muhimu katika kukuza uchumi jumuishi na wa watu wengi, sambamba na azma ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuhakikisha kuwa rasilimali za taifa zinawanufaisha Watanzania wote.

Akizungumza kuhusu ushiriki  wa Wizara  ya Madini  na taasisi  zake, Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Sehemu  ya Uendelezaji wachimbaji wadogo Mhandisi  Moses Kongola amesema wizara hiyo inasimamia na kuhakikisha  shughuli  za uvunaji  rasilimali madini unalinda mazingira kuwezesha shughuli  za kilimo na pia kutoa fursa ya wakulima kupima udongo kupitia maabara ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti  Tanzania.

Kwa upande wa STAMICO Meneja  wa Masoko  na Uhusiano, Deus  Alex  amesema Shirika linaweka nguvu katika utunzali wa mazingira  kwa kuongeza  uzalishaji wa nishati safi ya Rafiki Briquettes sambamba na kuendeleza  miradi yake ya uchongaji, uchimbaji, Uchakataji uongezaji thamani na uuzaji wa Madini.

Akiishukuru  Wizara ya Madini kupitia STAMICO Mwenyekiti wa Wanawake na Samia Dodoma, Fatuma  Madidi amesema Wanawake wamekuwa wanufaika  wa rasilimali madini kupitia bidhaa ya Rafiki Briquettes kwa kuwa imewapa fursa za kibiashara  katika  mikoa mbalimbali  ikiwemo Dodoma, Geita, Njombe, Mbeya na Shinyanga.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals