[Latest Updates]: Aliyoyasema Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde katika Kipindi cha Dakika 45 cha ITV, Machi 25, 2024 25,

Tarehe : March 26, 2024, 11:10 a.m.
left

Mada kuu ni Maendeleo ya Sekta ya Madini katika Miaka Mitatu ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan 

-    Eneo la kwanza lenye mafanikio makubwa ni ukusanyaji wa Maduhuli ya Serikali, katika kipindi cha miaka mitatu ya Mama mifumo ya ukusanyaji Maduhuli imeimarishwa katika Sekta ya Madini kufikia shilingi trilioni 1.9.

-    Eneo la pili ni Mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa umeongozeka sana katika kipindi hiki, mwaka 2018 Mchango wa Sekta ulikuwa ni asilimia 5.1, leo umefikia asilimia 9.1. Ilani ya Chama cha Mapinduzi imeelekeza kufikia mwaka 2025 Mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa ufikie asilimia 10.

-    Eneo la Tatu ni Uendelezaji wa Madini Mkakati/Muhimu ambayo Wizara imewekea mkakati, na uhitaji wake ni mkubwa duniani hivi sasa. Katika kipindi cha miaka mitatu ya Mama, Tanzania imesaini Mikataba kadhaa ili kuendeleza Madini hayo yanayopatikana kwa wingi nchini, na hivi karibuni Serikali kupitia Tume ya Madini imekabidhi Leseni kubwa ya Uchimbaji Madini Tembo (Heavy Mineral Sands) katika Eneo la Tajiri lililopo Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga, pamoja na Leseni ya Ujenzi wa Kiwanda cha Uchenjuaji wa Madini ya Metali wilayani Kahama mkoani Shinyanga. 

-    Pia, Miradi ya Madini Kinywe wa Godmwanga Gems uliopo Handeni Mkoani Tanga, Lindi Jumbo Mkoani Lindi, EcoGraf na Faru Graphite iliyopo Mahenge Mkoani Morogoro yote imesainiwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dkt. Samia. 

-    Eneo la Nne ni Uanzishwaji wa Masoko na Vituo vya Manunuzi ya Madini ambavyo vimerasimisha biashara ya Madini nchini, kwa mwaka wa fedha uliopita, Masoko 42 na Vituo vya Manunuzi ya Madini kiasi cha biashara iliyofanyika ni jumla ya shilingi trilioni 1.6 ikiwa ni matunda ya kurasimisha biashara ya madini. 

-    Eneo lingine ni Uendelezaji wa Wachimbaji Wadogo kwa kuwapatia maeneo na Leseni ili wafanye Uchimbaji bila usumbufu, pia kufikia mwezi Juni 2024 kutakuwa na jumla mashine 15 za Uchorongaji wa miamba na tayari mashine 5 zimeanza kuwanufaisha Wachimbaji katika Maeneo ya Chunya na Geita kwa gharama nafuu kupitia STAMICO kuliko zile za kampuni binafsi ikiwa ni juhudi za kuwajengea mazingira mazuri ya uchimbaji na uzalishaji.

-    Katika eneo hilohilo la Wachimbaji Wadogo, Wizara imekutana na taasisi za fedha na mabenki ili kuendelea kuwajengea uwezo na kuwafanya Wachimbaji hao kukopesheka kama Wajasiriamali kwani Sekta ya Madini imekuwa ikipata changamoto kubwa kukopesheka kutokana na asili yake. Baada ya Majadiliano hayo na mabenki kupitia mwavuli wao TBA sasa zitaanza kukopesha kundi hilo muhimu kwa masharti nafuu. 

-    Eneo lingine lenye mafanikio katika kipindi cha miaka mitatu ya Mama ni Utafiti wa kina wa jiosayansi kwa ajili ya kubaini kiasi cha Madini iliyopo hapa nchini, kupitia Vision 2030: Madini ni Maisha na Utajiri kwa kuimarisha GST ili kuwa na kanzidata ya kutosha kuhusu taarifa miamba ya yenye madini kutoka asilimia 16 zilizofanyiwa Utafiti huo hivi sasa hadi kufikia angalau asilimia 50 ifikapo mwaka 2030 pamoja na kuunganisha Sekta ya Madini na sekta zingine zikiwemo za Kilimo na Maji. 

-    Mwaka wa Fedha uliopita (2022/23) kupitia Tume ya Madini m Serikali imekusanya Maduhuli ya shilingi bilioni 678 ambapo asilimia 40 yametokana na Mchango wa Wachimbaji Wadogo wanaotumia zana duni, ndani ya mwaka huohuo Sekta ya Madini imetoa mchango mkubwa katika upatikanaji wa fedha za kigeni ambapo mauzo yaliyotokana na biashara ya madini yalikuwa ni dola bilioni 3.1 (trilioni 7.9).

-    Aidha, Mwaka wa fedha uliopita (2022/23) katika Mapato ya Kodi ya ndani, Sekta ya Madini imechangia shilingi trilioni 2.1 sawa na asilimia 15.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals