[Latest Updates]: Waziri Mavunde Azindua Kiwanda cha Uzalishaji Baruti na Vilipuzi - Kisarawe, Pwani

Tarehe : April 13, 2025, 9:09 p.m.
left

Kiwanda kuzalisha tani 22,000 za baruti na vilipuzi milioni 15 kwa mwaka

Ni matokeo ya kazi ya Rais Samia mazingira kuvutia uwekezaji

 Zaidi ya ajira 300 za moja kwa moja na 1000 zisizo za moja kwa moja kuzalishwa

KISARAWE, PWANI

Serikali inaendelea na utekelezaji wa mkakati wake wa kuhakikisha Tanzania inakuwa kitovu cha uzalishaji wa bidhaa zinazotumika migodini na kupunguza uagizaji wa bidhaa hizo kutoka nje ya nchi.

Hayo yamesemwa leo tarehe 13 Aprili, 2025 na Waziri wa Madini, Mh.Anthony Mavunde (Mb) alipotembelea na kuzindua kiwanda cha uzalishaji wa baruti na vilipuzi cha Solar Nitrochemicals Limited kilichopo Wilayani Kisarawe.

"Mh. Rais wetu Dkt. Samia S. Hassan anafanya kazi kubwa ya kufungua fursa na kuweka mazingira mazuri yanayovutia uwekezaji nchini. Matokeo ya kazi hiyo ni pamoja na ujenzi wa kiwanda hiki cha kuzalisha bidhaa hizi ambazo ni muhimu sana kwenye uchimbaji wa madini.

"Kama Serikali, tutaendelea kuwalinda wawekezaji wetu na kuwawekea mazingira wezeshi ili waendelee kuleta uwekezaji wenye tija utakaosaidia pia kuongeza mapato ya Serikali na ajira kwa watanzania.

 Matumizi ya baruti nchini ni tani 26,000 na vilipuzi pisi milioni 10 kwa mwaka, hivyo ujio wa kiwanda hichi kitakachozalisha tani 22,000 za baruti na vilipuzi pisi milioni 15 utasaidia kukidhi mahitaji ya ndani ya nchi na kuuza katika nchi zinazotuzunguka.

Uzalishaji wa baruti na vilipuzi ndani ya nchi utasaidia kupunguza gharama ya bidhaa hiyo kwa wachimbaji, ajira kwa wananchi na kuongeza ujuzi na elimu kwa watanzania.

Awali, Mkurugenzi Mkazi wa Kampuni ya Solar Nitrochemicals Limited, Bw. Kishor Bhomale alieleza kuwa ujenzi wa kiwanda hicho umegarimu Dola za Kimarekani Milioni 8 Sawa na Shilingi za Kitanzania bilioni 19 na wamelenga kuzalisha kwa ajili ya soko la ndani na nje ya nchi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mh. Petro Magoti alieleza kuwa uwepo wa kiwanda hicho utachochea ukuaji wa kiuchumi wa Kisarawe na pia wametenga eneo kubwa kwa ajili ya viwanda na kwamba wapo tayari kupokea wawekezaji katika ujenzi wa viwanda vya kuzalisha bidhaa mbalimbali.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals