[Latest Updates]: Kiwanda cha Kuchakata Chumvi Lindi Mbioni Kukamilishwa

Tarehe : June 12, 2025, 5:29 p.m.
left

Ruangwa, Lindi

Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ipo mbioni kukamilisha kiwanda cha kuchakata chumvi itakayozalishwa na wachimbaji wa chumvi katika  mkoa wa Lindi na Mtwara.

Hayo yamebainishwa leo Juni 12, 2025 na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Victoria Mwanziva wakati akifungua mafunzo ya namna bora ya kuzalisha chumvi ambayo yanaenda sambamba na maonesho ya madini na fursa za uwekezaji katika Sekta ya Madini wilayani Ruangwa.

Mwanziva ameeleza kuwa, kutokana na umuhimu wa kiwanda hicho matarajio ni kwamba  ifikapo mwezi Agosti 2025  kitakuwa kimekamilika na kuanza uchakataji mbalimbali ikiwa pamoja na kuiongezea thamani chumvi ghafi kutoka kwa wazalishaji.

Akibainisha kuhusu lengo la kufungua kiwanda hicho, Mwanziva amebainisha kuwa, Serikali imebaini changamoto zinazojitokeza kwa wazalishaji wa chumvi, huvyo imeona kuna kila sababu ya kufungua kiwanda kitakachopokea malighafi ya chumvi kutoka kwa wakulima na kuboresha kwa kuiongezea thamani ili zao hilo liwe na tija kwa wazalishaji na taifa kwa ujumla.

Mwanziva amefafanua kuwa, kiwanda hicho kitafanya kazi mbalimbali ikiwa pamoja na usafishaji na ufungaji wa chumvi, kitatoa mafunzo ya shamba darasa  ili kujenga uwezo kwa wakulima wa chumvi  pamoja na kununua chumvi ghafi kutoka kwa wazalishaji.

Kwa upande wake, Afisa Madini Mkazi (RMO) mkoa wa Mtwara Winfrida Mrema amesema kuwa, Serikali inatambua umuhimu wa madini ya chumvi nchini hivyo kupitia mafunzo hayo,  changamoto zote zilizotajwa zitawashirishwa kwa mamlaka husika ili kupata utatuzi wa haraka.

Naye, Mwakilishi kutoka Wizara ya Madini Mjiolojia Daniel Kidesheni amesema, Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) litaendelea kufanya tathimini katika mashamba ya chumvi katika mikoa ya kusini ili kuendelea kufahamu hali halisi ya mashamba na kuwasilisha taarifa ili kuweka mikakati bora ya kuongeza thamani ya chumvi nchini.

Awali, akielezea kuhusu mwenendo wa uzalishaji chumvi nchini mwakilishi kutoka  Chama cha Wazalishaji wa Chumvi Tanzani (TASPA) Ally Ismail , ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweza kulinda soko la ndani jambo ambalo  limeongeza tija kwa wazalishaji ukilinganisha na kipindi cha miaka ya nyuma.

Pamoja na pongezi hizo , Ismail ameiomba serikali kupunguza gharama za uagizaji wa madini joto  yanayotumika katika uboreshaji wa madini ya chumvi.

Kulingana na takwimu mahitaji ya chumvi nchini Tanzania  ni tani 200,000 kwa mwaka.

#MineralValueAddition
#InvestInTanzaniaMineralSector
#GDP:10.1%FromMineraSectorTz

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals