[Latest Updates]: Madini Yapongezwa kwa Kutoa Elimu na Kampuni ya GGML

Tarehe : July 11, 2023, 10:26 a.m.
left

#GGML wapongeza Mkaa mbadala wa STAMICO

#GGML Kinara uchangiaji huduma kwa jamii

Wizara ya Madini imepongezwa na  Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kutoa elimu kwa wananchi na wadau wanaotembelea banda la Wizara, taasisi zake na wadau wa Sekta ya Madini.

Pongezi hizo zimetolewa leo  Julai 11, 2023 na Mwanasheria Mkuu wa kampuni ya GGML  David Nzaligo alipotembelea banda la Wizara ya Madini (MADINI PAVILION) katika Maonyesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es salaam.

Akizungumza mara baada ya kutembelea banda la Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Nzaligo ameipongeza kampuni hiyo kwa kuleta Mkaa Mbadala wa Rafiki Briquettes ambao utasaidia kudhibiti uharibifu wa mazingira hapa nchini.
 
Akiwa katika banda la  kampuni ya GGML ambalo lipo pia ndani ya banda la madini, Nzaligo amewapongeza wafanyakazi wa GGML na kampuni zingine ndani ya banda hilo kwa kuonyesha weledi mkubwa katika kutoa elimu ya shughuli wanazozifanya ikiwemo uchimbaji madini na mnyororo wake.

"Nafahamu GGML wapo vizuri kwenye miradi mingi ya kijamii pamoja na uwezeshaji wananchi kiuchumi. Nafurahi kwamba  mafanikio hayo wanayaelezea vizuri kwa kila mwananchi anayetembelea banda la GGML," alisema.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals